Shirikisho la Kandanda Africa (CAF) limesema kuwa
mashindano yajayo yatafanyika nchini Cameroon kati ya Januari 9 mpaka Februari
6.
Kwa mujibu wa CAF uamuzi huo umefikiwa baada ya kupata
ripoti kutoka Cameroon zinazoeleza kuwa kipindi cha Juni kitakuwa kigumu kwa
hali ya hewa.
Mabadiliko hayo pia yanamaanisha kuwa mashindano ya
Afrika hayataangukia katika wakati sawa na mashindano ya kombe la dunia la
vilabu litakalofanyika Uchina Juni 2021.
Kurudishwa kwa majira hayo ya Januari mwaka 2021 kumeibua
mjadala wa kandanda baina ya Afika na Ulaya.
Mwezi Januari ni kipindi ambacho ligi za Ulaya
zinakuwa katikati na ushindani unakuwa mkubwa, hivyo makocha wengi hawafurahii
kuwaachia wachezaji wao nyota kurejea Afrika.
Wachezaji hao nyota wa Afrika hukaa mpaka wiki tano na
timu zao za taifa na hukosa mpaka michezo mitano ya ligi na klabu zao.
Mwezi Juni nikipindi kinachopendwa kwa kuwa ligi
nyingi za Ulaya huwa kwenye mapumziko.
"Kwa kweli ratiba hiyo (ya mwezi Januari)
inakuathiri mno unapofikiria kuwasajili wachezaji kutoka Afrika," kocha wa
zamani wa Tottenham Harry Redknapp ameiambia BBC.
"Na kwa hakika (wakirudi) baada ya michuano
wanakuwa si kama walivyoondoka. Huwa hawarudi katika kiwango chao baada ya
mashindano," amesisitiza.
Vinara wa Ligi ya EPL Liverpool mathalani wanaweza
kuwakosa nyota wao tegemezi watatu kutokana na mabadiliko hayo mwakani ambao ni
Sadio Mane, Mohamed Salah na Naby Keita kwa mwezi mmoja.
0 Comments:
Post a Comment