Januari 5, 2010 klabu ya DC United ya nchini Marekani
iliingia mkataba na nahodha wa zamani wa klabu hiyo Ben Olsen ili awe kocha
msaidizi wa miamba hiyo.
Miezi saba ijayo alikuwa kocha mkuu wa klabu hiyo yenye
maskani yake jijini Washington D.C Nahodha huyo wa zamani alihudumu na DC
United akiwa mchezaji mnamo mwaka 1998 ikiwa ni miaka mitatu baada ya kuwapo na
timu ya Chuo Kikuu cha Virginia wakati
huo kocha wake Bruce Arena alikuja baadaye kuhudumu na DC United.
Wakati anatua mwaka huo ndiyo waliofanikiwa kutwaa taji la
Ligi ya Mabingwa kwa Amerika ya Kaskazini na Copa Interamericana huku Olsen
akitajwa kuwa mchezaji chipukizi wa msimu huo aliyefanya vizuri. Katika msimamo
wa MLS walishika nafasi ya pili.
Mwaka uliofuata walishinda taji la MLS. Pia walifanya hivyo
mnamo mwaka 2004 na mnamo mwaka 2008 D.C United ilitwaa US Open.
Majeruhi yalimfanya Olsen astaafu mnamo mwaka 2009 akiwa
amecheza mechi 221 za ligi. Baada ya hapo alikaa muda mfupi kama kocha msaidizi
wa kocha mkuu wa Curt Onalfo.
Hata hivyo Agosti 2010 walianza vibaya hivyo walimtimua
Onalfo na kumtangaza Olsen kuwa kocha wa mpito.
Mpaka sasa anaendelea kuinoa DC United. Wayne Rooney ni miongoni mwa
wachezaji waliofaidi wakiwa na Olsen msimu wa 2018-19 akicheza mechi 48 na
kufunga mabao 23.
0 Comments:
Post a Comment