Saturday, January 25, 2020

UN yataka usaidizi kukabiliana na nzige Afrika Mashariki


Umoja wa Mataifa umetoa wito wa usaidizi wa kimataifa kukabiliana na nzige wengi waliovamia maeneo ya Afrika mashariki.

Msemaji wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa mataifa (FAO), ametoa wito wa kutolewa kwa msaada ili kukabiliana na athari za nzige kama vile ukosefu wa chakula, utapiamlo na kuathirika kwa mfumo wa maisha ya kila siku.

Ethiopia, Kenya na Somalia zinapitia wakati mumu kukabiliana na na makundi ya nzige ambako hakujawahi kutokea hapo kabla kunakoathiri mazao ya kilimo, limesema shirika la FAO.

Shirika hilo linahofia kwamba idadi ya nzige hao huenda ikaongezeka mara 500 zaidi ifikapo Juni mwaka huu.

Kwa siku moja tu, kundi la nzige Paris huenda likala kiwango cha chakula kinachoweza kuliwa na nusu idadi ya watu wote Ufaransa.

Nzige wanaweza kusafiri umbali wa kilomita 150 (maili 93) kwa siku na kila nzige mkubwa anaweza kula chakula kiasi kikubwa tu cha chakula kwa siku.

Tatizo hilo linaendelea kuwa kubwa zaidi kadiri siku zinavyoendelea. Mbali na nzige hao kuongezeka maeneo ya Afrika Mashariki, pia wamejitokza katika nchi za India, Iran na Pakistan, ambao huenda wakabadilika na kuanza kusambaa kwa makundi ifikapo msimu wa chipukizi


0 Comments:

Post a Comment