Januari 16, 2010 mchezaji
wa Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi alifikisha mabao 100 akiwa na
miamba hiyo ya Katalunya hivyo kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri
mdogo katika historia ya klabu hiyo kufikisha idadi hiyo ya mabao.
Bao hilo la
mia moja alilifunga katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania dhidi ya Sevilla
katika dimba la Camp Nou.
Timu hizo mbili zilikuwa zimekutana mara mbili ndani
ya siku 30 katika Kombe la Mfalme hatua ya 16 bora huku Sevilla ikisonga mbele
kwa uwiano wa mabao ya ugenini baada ya uwiano wa mabao 2-2.
Katika mzunguko wa
pili Barcelona ilishinda 1-0 huku mlinda mlango wa Sevilla wakati huo Andres
Palop aliokoa michomo aliyokuwa akiitupa langoni hapo. Katika mchezo wa La Liga,
Palop alilinda lango lake vizuri hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna
nyota yeyote wa Barcelona aliyefanikiwa kuchungulia nyavu zake.
Katika dakika
ya 49 bao la kujifunga la mlinzi wa kati Julien Escude lilitosha kuanza
kufungua milango ya kugusa nyavu zake.
Pedro Rodriguez aliongeza idadi ya mabao
katika dakika ya 70 ya mchezo huo; hatimaye Lionel Messi katika dakika ya 84
alitupia bao la tatu katika mchezo huo kwenye ushindi wa mabao 4-0. Messi
aliweka rekodi hiyo akiwa na miaka 22, miezi sita na siku 22.
0 Comments:
Post a Comment