Januari 9, 2012 alifariki
dunia mwanasiasa aliyehudumu katika taifa la Guinea Bissau akiwa Rais; Malam Bacai
Sanha.
Alifariki dunia jijini Paris nchini Ufaransa alikopelekwa kwa ajili ya
matibabu. Mnamo Novemba 2011 kiongozi huyo wa juu katika taifa hilo alisafiri
kwenda Ufaransa kwa ajili ya kuangalia afya yake ambayo haikuwekwa wazi huku
taarifa za ndani zikieleza kuwa alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kisukari.
Aidha hapo awali aliwahi kwenda nchini Senegal kwa ajili ya kuchunguza afya
yake. Ikulu ya Guinea Bissau ilitangaza kwa uchungu na majonzi kuwa Malam Bacai
Sanha amefariki dunia katika hospitali ya kijeshi ya Val-de-Grace jijini Paris.
Tangu alipochaguliwa mwaka 2009 kushika madaraka hayo ya juu alikuwa akipata
matibabu ya mara kwa mara na kwamba katika dakika za mwishoni katika kuupigania
uhai wake alishindwa kabisa kuzungumza.
Veteran huyo wa kivita alishindwa mara
mbili kuchaguliwa kabla ya mwaka 2009, akijaribu uchaguzi wa mwaka 2000 na ule
wa 2005.
Alizaliwa Mei 5, 1947 katika mji wa Darsalame, wakati huo ikiitwa
Portuguese Guinea.
Enzi za utawala wake alijitahidi kuliweka taifa hilo katika
hali ya utulivu baada ya kuuawa kwa Rais João Bernardo Vieira.
Hata hivyo Malam
Bacai Sanha alishindwa kuzuia biashara ya dawa za kulevya, rushwa na vurugu za
hapa na pale. Hali ya mbaya katika utoaji wa huduma za afya na safari za nje za
mara kwa mara kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake kuliiacha Guinea Bissau
katika wakati mgumu.
Aliingia katika siasa za nchi hiyo akiwa bado kijana kwa
tiketi ya chama cha mrengo wa kushoto cha African ambacho kilipambana kulilitea
taifa la Guinea Bissau na Cape Verde uhuru wao kutoka kwa Wareno mnamo mwaka
1974 walifanikiwa.
Alishawahi kushika nyadhifa nyingine za kisiasa katika taifa
hilo la Guinea Bissau.
0 Comments:
Post a Comment