Son Cubano ni aina nyingine ya muziki wa Cuba ambayo asili yake ni katika sehemu za milimani huko Mashariki mwa Cuba.
Aina hii ya muziki ilianza kuwika katika karne ya 19 ikiwa na vionjo vya Kihispaniola na Kiafrika. Miongoni mwa vionjo kutoka Hispania ni upangiliaji wa sauti, vina na mizani vyote vimechukuliwa kutoka katika gitaa la Kihispaniola.
Kwa upande mwingine kuna vifaa vingine kama Clave, bongo, marcas na vingine vya percussion vyote vina mizizi kutoka utamaduni wa Kibantu.
Mwanzoni mwa miaka ya 1900 aina hii ya muziki ilikuwa imefika mjini Havana ambako rekodi ya kwanza ilitengenezwa mnamo mwaka 1917. Hatua hiyo ya kurekodi muziki wa son katika studio zilizokuwapo mjini Havana ilitoa mwanya wa aina hii ya muziki kusambaa katika maeneo mbalimbali ya kisiwa hicho na ulianza kuwa maarufu na wenye ushawishi.
Makundi ya mwanzo ya wanamuziki huo yalikuwa na wasanii watatu hadi watano lakini kuanzia miaka ya 1920 wanamuziki sita wenyewe hupendelea kuita 'Sexteto' mfumo ambao umekuwa ukitumiwa.
Mnamo miaka ya 1930 bendi nyingi za muziki wa Son Cubano waliingiza kifaa kingine cha muziki ambacho ni tarumbeta (tarumbeta) hivyo kuwa na idadi ya wanamuziki saba (Septetos).
Miaka 1940 son cubano waliongeza vifaa vingine ikiwamo kinanda, congas na hivyo imekuwa ndio ustaarabu wa muziki wa son cubano: cunjunto.
Hivyo basi uwepo wa aina hii ya muziki inaangaziwa zaidi kutoka miaka ya 1930 wakati ambapo bendi nyingi zilikuwa zikienda kufanya ziara barani Ulaya na Amerika Kaskazini.
Katika redio huko Afrika Magharibi na maeneo ya Kongo muziki wa son Cubano ulikuwa ukipigwa. Son Cubano ndiyo imekuwa na ushawishi mkubwa katika uanzishwaji wa aina nyingine ya muziki wa rumba kutoka ardhi ya Kongo.
Mnamo miaka ya 1960 son cubano ilisababisha kuendelea kwa haraka kwa aina ya muziki wa Salsa katika jiji la New York nchini Marekani kwani wasanii wa Purto Rico walichanganya na vionjo vingine vya Latini Amerika.
Wakati salsa ikipata umaarufu wa kimataifa katika nusu ya pili ya karne ya 20 Son Cubano ilikuwa imejiingiza katika muundo mwingine kama songo na timba ambapo ilikuwa ikifahamika kwa jina la 'Cuban Salsa'
Imetayarishwa na Jabir Johnson......XVII-I-MMXX

0 Comments:
Post a Comment