Monday, January 27, 2020

Kifo cha Suharto (1921-2008)

Januari 27, 2008 alifariki dunia mwanasiasa maarufu wa Indonesia ambaye aliwahi kushika wadhifa wa kuliongoza taifa hilo akiwa Rais wa pili. Huyu anafahamika kwa jina la Suharto. Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 86. 

Aliliongoza taifa hilo kutoka Machi 27, 1968 hadi alipojiuzulu Mei 21, 1998. Baada ya kujiuzulu nafasi ya kuliongoza taifa hilo Suharto alikuwa akilazwa mara kwa mara kutoka na kukabiliwa na stroke, maradhi ya moyo na matatizo ya utumbo. 

Hata wanasheria wake waliwahi kuwasilisha kwa Mwanasheria Mkuu kuwa hali yake sio nzuri kwa hiyo hatakuwa na uwezo wa kusimama kizimbani kujibu mashtaka yaliyokuwa yakimkabili. 

Mnamo mwaka 2006 mwanasheria mkuu Abdurrahman alituma timu ya madaktari 20 ili wafanya uchunguzi wa kina kuhusu afya ya Suharto. Daktari mmoja aliyefahamika kwa jina la Brigedia-Jenerali Marjo Subiandono alikaririwa akionyesha wasiwasi wake kwa kusema Suharto ana matatizo mawili katika ubongo wake. 

Hata hivyo Januari 4, 2008 Suharto alichukuliwa kwenda katika Hospitali ya Pertamina jijini Jakarta kutokana na hali yake ya afya kuwa dhaifu kwani alikuwa amevimba mikono, miguu na tumbo; pia inaelezwa Suharto alikuwa na matatizo japo sio kwa sana katika figo zake. 

Hali ilizidi kuwa dhaifu kwani majuma kadhaa baadaye kulijitokeza anaemia, shinikizo la damu la kushuka kutokana na maradhi ya moyo na figo pia kuvunja kwa damu kwa ndani, mapafu kujaa maji, damu katika haja kubwa na ndogo ambayo ilisababishwa na kushuka kwa kiwango cha haemoglobin. 

Januari 23, 2008 hali ya Suharto ilikuwa mbaya zaidi kwani ilijitokeza hali kwa kitaalamu hufahamika kama Sepsisi ambayo mwili huwa unaachia keemikali kwa wingi ili kupambana na maradhi hivyo kemikali hiyo ikisambaa mwili mzima huleta madhara makubwa kwani kila eneo litakuwa halijiwezi. 

Familia ya Suharto ilikubaliana na kuwataka madaktari kuondoa vifaa vya usaidizi alivyokuwa amewekewa na ilipofika Januari 27, 2008 saa 7:09 mchana Suharto alifariki dunia. 

Dakika chache baada ya taarifa za kifo chake Rais wa Indonesia wakati huo Susilo Bambang Yudhoyono aliita waandishi wa habari na kutangaza kifo hicho huku akimwelezea Suharto kuwa ni miongoni mwa watoto bora wa Indonesia na kuwataka raia wa taifa hilo kutoa heshima kwa rais huyo wa zamani bila kujali madhaifu yaliyojitokeza wakati wa utawala wake. 

Mwili wa Suharto ulichukuliwa kutoka Jakarta hadi Giri Bangun jijini Solo katika jiji la Central Java na kuzikwa huko. Suharto alizikwa pembezoni mwa kaburi la mkewe kwa heshima zote za kijeshi. 

Rais Yudhoyono na maofisa wa serikali walihudhuria mazishi hayo huku watu wa Indonesia wakisimama katika mitaa na barabarani kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo. Rais Yudhoyono alitangaza juma moja la maombolezo kutokana na kifo cha Suharto.

Alizaliwa Juni 8, 1921 katika kijiji cha Kemusuk kilichokuwa katika dola ya Yogyakarta. Suharto alizaliwa wakati wa utawala wa Wadachi katika Indonesia wakati huo ikiitwa Dutch East Indies. 

Alizaliwa katika familia maskini iliyokuwa ikiishi katika nyumba iliyojengwa kwa miti ya mianzi na kusilibwa na udongo katika ardhi ya Wajava. Kiongozi huyo wa kijeshi aliingia madarakani  baada ya kumtoa madarakani Sukarno ambaye alikuwa Rais wa kwanza wa taifa hilo. 

Alianza kushikilia hatamu tangu mwaka 1967 hadi alipojiuzulu mwaka 1998. Katika hotuba yake ya kujiuzulu aliowaomba radhi watu wa Indonesia kwa makosa ambayo aliyafanya wakati wa utawala wake.

Suharto alizaliwa katika kijiji kidogo cha Kemusuk karibu na jiji la Yogyakarta. Alikuwa katika hali ya unyenyekevu. Wazazi wake wa Kijava waliokuwa waumini wa dini ya Kiislamu walitalikiana na kusalia kama wadaawa muda mfupi baada ya Suharto kuzaliwa. 

Wakati wa utawala wa Wajapani katika Indonesia, Suharto alihudumu katika Jeshi la Ulinzi la Wajapan. Wakati wa harakati za kupata uhuru kwa taifa hilo alikuwamo katika Majeshi ya Indonesia. Suharto alifanikiwa kupanda cheo na kuwa Meja Jenerali baada ya Uhuru wa Indonesia. Alifanya jaribio la kupindua utawala wa Sukarno (mwasisi wa taifa hilo) na kufanikiwa Septemba 30, 1965 akiungwa mkono na Chama cha Kikomunisti cha Indonesia. 

Aliteuliwa kushika nafasi ya urais baada ya jaribio hilo mwaka 1967 na mwaka 1968 alichaguliwa kuwa Rais wa taifa hilo. 

Aliposhika madaraka hiyo alianza kuongoza taifa hilo kwa kuweka sheria ambazo zilikuwa zikimpa kuitambulika na raia wa taifa hilo. 

Suharto alikuwa imara miaka ile ya 1970 hadi 1980. Mwanzoni mwa miaka ya 1990  hali ilikuwa mbaya katika taifa hilo, ambalo inaelezwa udikteta ulitawala  na vitendo vya rushwa. Hali hiyo ilimlazimisha kujiuzulu May 1998. 

Wakati wa kujiuzulu kwake aliomba msamaha kwa Waindonesia wote kwa yaliyotokea kwani yalisababisha uchumi wa taifa hilo kubaki nyuma. 

0 Comments:

Post a Comment