Januari
3, 2008 alifariki dunia mwanamasumbwi wa Korea Kusini Choi Yo Sam.
Bondia huyo
katika sikukuu ya Christmas ya mwaka 2007 alifanikiwa kuutetea mkanda wa WBO
Intercontinental katika uzito wa FLY kwa pointi (UD baada ya kumzabua Heri Amol
wa Indonesia.
Katika raundi ya 12 Choi aliangushwa zikiwa zimesalia sekunde
tano licha ya kuangushwa hatimaye alifanikiwa kushinda pambano hilo. Choi Yo-Sam
alizimia wakati akiwa katika ulingo siku hiyo hivyo alichukuliwa na kukimbizwa
katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Soonchunhyang ili aweze kufanyiwa upasuaji
wa ubongo.
Januari 2, 2008 ilitangazwa kwamba ubongo wa bondia Choi Yo-Sam
ulikuwa umeshashindwa kuendelea kufanya kazi licha kwamba alikuwa anathema hatimaye
Januari 3, 2008 akafariki dunia wakati ambapo aliondolewa vifaa vya oksijeni
alivyokuwa akivitumia.
Baada ya kifo hicho Wasanii wawili waliokuwa wakiunda kundi
la LeesSang wa Korea Kusini Kang Hee-gun na Gil Seong-joon waliipa albamu yao
ya tano jina la CHAMPION na kuidedicate kwa bondia huyo kutokana na kifo hicho.
Hata hivyo familia ya Choi ilitoa viungo vya bondia huyo kwa wagonjwa sita
waliokuwa na uhitaji. Kwa kitendo hicho serikali ya Korea Kusini ilimpa medali
Choi Yo-Sam.
Kifo cha mwanamasumbwi huyo kinafanana na kile cha mwaka 1982
kwenye pambano baina ya bingwa wa uzito mwepesi Ray ‘Boom Boom’ Mancini wa
Marekani na Kim Duk-koo wa Korea Kusini ambaye alifariki dunia kutokana na
majeraha katika kichwa.
Choi
aliingia katika ndondi za kimataifa mnamo mwaka 1993 na kushinda mikanda miwili
ya Lineal na WBC katika uzito mwepesi wa FLY mnamo mwaka 1999 dhidi ya Saman
Sorjaturong.
Pia alifanikiwa kutetea mikanda yake mara tatu kabla ya kupoteza
kwa Jorge Arce wa Mexico katika raundi ya sita kwa KO mnamo mwaka 2002.
Mnamo
mwaka 2003 alipoteza dhidi ya Beibis Mendoza katika Interim WBA. Mwaka 2004
alipata katika uzito akipambana na Lorenzo Parra kuwania WBA uzito wa FLY.
Choi
alizaliwa Machi 1, 1972 huko Jeongeup,
Jeollabukdo Korea Kusini.
0 Comments:
Post a Comment