Januari 10, 2010 mwanadada mchezaji
wa kandanda kutoka nchini Brazil Marta Vieira da Silva, alitwaa tuzo ya
tano ya mchezaji bora wa mwaka wa
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Baada ya kumaliza nafasi ya tatu mnamo
mwaka 2004 katika upigaji wa kura na kushika nafasi ya pili mnamo mwaka 2005
Marta alishinda tuzo yake ya kwanza ya FIFA mnamo mwaka 2006.
Alishinda tuzo
hiyo wakati huo akihudumu na klabu ya Umea iliyopo nchini Sweden. Pia alichukua
tuzo hiyo mnamo mwaka 2007 na mara ya
tatu alifanikiwa kuchukua tuzo hiyo mwaka 2008.
Mnamo mwaka 2009 aliondoka
nchini Sweden na kwenda zake nchini Marekani katika klabu ya Alos Angeles Sol
ambako alimaliza msimu huo akiwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya soka ya wanawake.
Msimu huo huo alichukua tuzo ya FIFA rekodi ambayo Lionel Messi wa Argentina na
klabu ya Barcelona aliifikia mnamo mwaka 2012.
Akiwa na Los Angeles Januari ya
2010 alipata dili jingine la kujiunga na FC Gold Pride ambako aliibuka tena
kidedea kwa kufumania nyavu na kuisadia kutwaa taji la msimu huo la WPS katika
ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya
Philadelphia Septemba 26.
Miezi miwili baadaye alitajwa kuwa mchezaji bora wa
mwaka kwa mara ya tano akiweka rekodi hiyo mpya. Mnamo mwaka 2011 na 2012
alimaliza katika nafasi ya pili katika upigaji wa kura akizidiwa na raia wa
Japan Homare Sawa na Mmarekani Abby Wambach.
Alizaliwa Februari 19, 1986 Dois
Riachos, State of Alagoas, Brazil.
0 Comments:
Post a Comment