Mbio za Magari maarufu
Dakar Rally zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumapili hii nchini Saudi Arabia.
Mbio hizo mwaka huu ni toleo la 42 ambapo mwaka huu zitaanzia mjini Jeddah na
kumalizika Januari 12 mjini Qiddiya.
Dakar Rally mwaka huu itapita katika hatua
12 ambako kutashuhudia madereva pikipiki, malori, magari na pikipiki za matairi
manne maarifu Quads wakionyesha uwezo.
Dakar Rally ni mashindano magumu ya
vifaa vya moto katika ardhi ambapo mwaka huu madereva 400 watapambana na nusu
ya hao watapambana katika ardhi yenye mchanga.
Dakar Rally huchukua takribani
kilometa 7,500 katika kategori tano ikiwamo UTV’s
0 Comments:
Post a Comment