Tuesday, December 11, 2018

Daei: Iran inaweza kukutana na Japan mataifa ya Asia 2019

Ali Daei

DEC. 11, 2018 - Mkongwe wa kandanda nchini Iran Alli Daei amesema taifa lake linaweza kukutana katika fainali na Japan katika michuano ya Mataifa ya Asia yanayotarajiwa kuanza Januari 5 kwenye ardhi ya Falme za Kiarabu. 

Daei anasema Japan ilionyesha mpira mkubwa katika Kombe la Dunia nchini Russia sawa na Iran. Hata hivyo nyota huyo anayeongoza kwa ufungaji wa mabao wa mashindano hayo akifunga mabao 14 katika mara tatu alizoshiriki akiwa na Iran amewataja nyota wa kikosi cha kocha Melli, Alireza Jahanbakhsh, Saman Ghoddos, Mehdi Taremi na Sardar Azmoun kuwa ni muhimu katika kuipeleka Iran fainali za michuano hiyo hapo mwakani. 

Iran ni mabingwa mara tatu wa Kombe la Mataifa ya Asia kwa mara ya mwisho ilitwaa taji hilo mwaka 1976.

0 Comments:

Post a Comment