Mshambualiaji Gareth Bale wa Real Madrid, ameonyesha nia ya
kutaka kuondoka na kiatu cha dhahabu katika mashindano ya Fainali ya Klabu
Bingwa ya Dunia.
Mshambuliaji huyo juzi alifunga mabao matatu 'hat-trick' na
kuiwezesha timu yake kuizamisha Kashima Antlers ya Japan kwa mabao 3-1 katika
mechi ya nusu fainali na sasa itacheza fainali na wenyeji Al Ain ya Umoja wa
Falme za Kiarabu.
Kocha wa Real, Santiago Solari, amemfagilia Bale, ambaye
amefikisha mabao sita katika mechi tano walizocheza hadi sasa, huku Real
ikiwania kutwaa taji la tatu mfululizo la michuano hiyo.
Mechi ya fainali
itachezwa kesho kwenye Uwanja wa Zayed Sports City, mchezo unaoonekana kuvuta
hisia za wengi ikizingatiwa Al Ain ya Abu Dhabi iliwaduwaza wengi baada ya
kuing'oa kwa changamoto ya mikwaju ya penati bingwa wa Amerika ya Kusini, River
Plate ya Argentina.
Kocha Santiago Solari akizungumza jambo na Gareth Bale baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Kashima Antlers. Bale alifunga 'hat trick' |
0 Comments:
Post a Comment