Wednesday, February 8, 2017

Mbowe atajwa kuhusika dawa za kulevya

NA MWANDISHI WETU
Freeman Mbowe
MWENYEKITI wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni Dodoma na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe ametakiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kufika katika kituo kikuu cha Polisi kwa ajili ya mahojiano kuhusu dawa za kulevya.

Wengine waliotajwa ni mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddi Azzan ambaye alikuwa kipa wa timu ya wabunge na timu ya wabunge wa Simba wakati alipokuwa mbunge,  Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji.

Akizungumza ofisini kwake leo, Makonda ametaja orodha ya majina kadhaa marufu kati ya 65 amedai wanatakiwa kufika katika kituo cha polisi kwa ajili ya zoezi hilo la mahojiano katika kampeni yake ya kuendeleza kupambana na utumiaji na biashara ya dawa ya kulevya.

Majina mengine maarufu yaliyopo katika orodha hiyo ni na mfanyabiashara maarufu wa nguo Hussein Pambakali,  Mchungaji Josephat Gwajima na wamiliki wa Slipway na Yatchy Club. .

Makonda ameielezea orodha hiyo kuwa ni ya wale ambao wanasadikiwa kujihusisha na biashara hiyo.


0 Comments:

Post a Comment