NA MWANDISHI WETU
January Makamba |
SERIKALI imewataka wazalishaji
na wafanyabiashara kuacha kuilalamikia kwa hatua iliyochukua ya
kutangaza marufuku ya uzalishaji, usambazaji na matumizi ya viroba kuwa imekuja
ghafla huku wakijua kwamba tamko hilo
lilitolewa tangu Mei mwaka jana.
Hayo yanajiri ikiwa imebaki siku moja kuanza marufu ya
uzalishaji,uingiaji, usambazaji na matumizi ya viroba pamoja na pombe kali
nchini.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba amesema mpaka
sasa serikali imepokea maombi ya wazalishaji tisa pekee ambao wameonyesha
ushahidi wa kuelekea kuhamia kwenye teknolojia ya chupa na hivyo watahitaji
muda mchache kufanya hivyo na ambao watatimiza masharti na kupata kibali
maalum.
Makamba amesema serikali imekuwa ikipoteza shilingi bilioni 600
kutokana na ukwepaji kodi na
utengenezaji wa viroba hivyo kufuatia katazo hilo litakaloanza rasmi
kesho itakuwa mkakati wa kupunguza upatikaji wake kirahisi ili kiwango cha
unywaji wa viroba kwa watanzania kiendane na mapato ya taifa, kulinda afya ya
jamii pamoja na uhifadhi wa mazingira.
Aidha wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa
zoezi hilo la
upigaji marufuku matumizi ya viroba kwa kutoa taarifa kwenye vyombo husika ili
wale wanaozalisha, kuuza na kuhifadhi waweze kuchukuliwa hatua stahiki na
zawadi kutolewa kwa watakaotoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwao.
0 Comments:
Post a Comment