NA
MWANDISHI WETU
Sukari ya Kilombero katika pakiti zake |
Zaidi ya shilingi milioni tisa zimekusanywa na
wakala wa vipimo mkoani Mbeya baada ya
kupigwa faini wafanyabiashara waliokamatwa wakiuza sukari iliyofungashwa
katika ujazo usiokubalika kisheria.
Kwa mujibu wa sheria ya vipimo ya mwaka 2002 sura
namba 340; ufungashaji, usafirishaji na uuzaji wa bidhaa yoyote katika ujazo
usio stahili ni kosa na adhabu yake ni faini kuanzia shilingi laki moja mpaka
shilingi milioni 20.
Meneja wa Kanda Richard Mbonabucha amesema wafanyabiashara
kumi na wawili wamekamatwa katika operesheni ya kukamata bidhaa zinazofungashwa
kinyume na taratibu iliyoanza jana mkoani humo.
Amesema baada ya kukamatwa na kukiri makosa
wafanyabiashara hao wametozwa faini ya kati ya shilingi laki tano na shilingi
milioni moja kwa kuwa ni kosa lao la kwanza na kwamba watakaporudia kosa hilo hawatatozwa faini na
badala yake watafikishwa mahakamani.
Meneja huyo wa wakala wa vipimo mbeya ametoa
tahadhari kwa wananchi juu ya matumizi wa bidhaa zisizo la nembo ya ubora wala
mahala inapozalishwa kama ilivyo kwa sukari
iliyo kamatwa.
Baadhi ya wafanyabiashara waliokamatwa wamesema
sukari hiyo inafungashwa kwenye vifuko vinavyoonyesha kuwa ni gramu mia tano
lakini kiuhalishia ni kati ya gramu 320 na 350 na kwamba wao wanaipata kutoka
kwa wafanyabiashara waliowataja kwa jina maarufu la Njemke.
0 Comments:
Post a Comment