Thursday, February 9, 2017

Gwajima: Makonda hajakomaa...chuki tu

NA MWANDISHI WETU
Askofu Gwajima baada ya kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari
ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Mchungaji Josephat Gwajima amemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Joseph Magufuli kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amtoe katika ngazi hiyo ya uongozi na kumpangia kazi nyingine ili kunusuru uhai wa nchi.
Aidha Askofu Gwajima amesema kuna dhana imejengeka miongoni mwa watanzania kuwa kila kitu ambacho anakitenda Makonda ametumwa na Rais Magufuli.
Katika  mkutano wake na waandishi wa habari asubuhi ya leo kanisani kwake Ubungo jijini Dar es Salaam Askofu Gwajima amesema Makonda ameufanya mfumo wa uongozi nchini kupooza hivyo kushindwa kuunga mkono anayoyafanya kutokana ukaribu wake na Rais wa nchi.
“Makonda ni Mchapakazi lakini Mambo ya Utawala hawezi, namuomba rais amtafutie kazi nyingine, nashauri umtafutie kazi nyingine, sio umfukuze,” alisema Askofu Gwajima.
“Nani anatakiwa kuniita mimi kama Askofu Mkuu Polisi? Ni Polisi sio Makonda. Makonda anajiona kama Mkuu wa Wakuu wa Mikoa yote na Mawaziri wote. Sio desturi ya rais hata kidogo eti awatenge mawaziri wake eti aongee na Makonda. Rais alikuwa anampongeza Makonda kwa sababu kafanya vizuri. Makonda ana ujasiri na anajituma hivyo rais kumpongeza ni halali. Makonda anaweza kuwa Kiongozi mkuu siku zijazo kama akiondoa baadhi ya hitilafu,” alisema Askofu Gwajima.
Gwajima amehoji ujasiri wa Makonda kumkemea Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Kamanda wa Kanda Maalum Simon Sirro.
Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima
Hata hivyo Gwajima amesema wivu na chuki binafsi alizonazo kwa ajili ya mafanikio ya wengine ni vema akajipambanua na kuachana nayo kama anataka kuwa salama katika nafasi yake.
“Namuomba rais amkanye Makonda. Chuki zake binafsi za mtu mmoja mmoja asiziingize kwenye system ya serikali ni hatari sana,…Juzi kati tulikuwa na mechi kati ya maasikofu na viongozi, Mimi nilikuwa namba tia yeye namba 10. Alikuwa ananiangalia jicho baya sana. Mimi, Makonda, Kamanda Sirro Spika wa Bunge tulikuwa tuna mechi si angenikamata hapo?,”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili inayoshirikisha viongozi wa dini nchini, Askofu William Mwamalanga amesema wanaunga mkono juhudi za kupinga dawa za kulevya lakini kwa walipofikia sasa sio sawasawa ni katika kuchafuana hali ambayo haitaweza kufanikisha vita hiyo ngumu.

Gazeti la Mwananchi Februari 9, 2017

Gazeti la Tanzania Daima Februari 9, 2017


0 Comments:

Post a Comment