Robert Mugabe |
Kiongozi huyo aliyepo madarakani tangu
walipojipatia uhuru mwaka 1980 amekaririwa akisema wanaopaswa kusema aondoke
madarakani ni chama chake, lakini mpaka sasa Kamati Kuu imemtaka asimame kwa
ajili ya uchaguzi mkuu ujao.
Mugabe ambaye amekuwa mahiri kwa kauli kali
ameongeza walio wengi katika nchi yake wanataka aendelee kwani hawaoni mbadala
wa atakayepokea kijiti.
Hata hivyo amekana kuwa na matatizo ya kiafya
licha ya kuwa na safari za mara kwa mara za kwenda Dubai
na Singapore .
Katika hotuba amekuwa akisoma kwa muda mfupi na
taratibu tofauti na walivyozoea. Ikumbukwe Septemba mwaka jana alisoma hotuba
ambayo ilikuwa sawa na ile aliyoitoa mwezi mmoja kabla bila kujua, hali
iliyoibua maswali kuhusu hali yake ya afya.
Aidha Mugabe alimsifia Rais wa Marekani Donald
Trump kwa kuendelea kuimarisha sera za utaifa ambazo ameziita kuwa ni muhimu
kwa maendeleo ya Zimbabwe .
Mugabe ambaye ni mwenyekiti wa ZANU-PF atasimama
kwa uchaguzi wa mwaka 2018, ambapo juma lililopita mkewe Grace Mugabe aliibuka
na kusema kuwa anaweza kuwa mtangulizi wake huku akikaririwa kwa kauli tata
kuwa endapo Mungu ataamua Mugabe kufa basi wataipitisha maiti yake ipigiwe
kura.
Endapo kiongozi huyo atachaguliwa na kumaliza muhula wake mwingine atafikisha miaka 100.
Endapo kiongozi huyo atachaguliwa na kumaliza muhula wake mwingine atafikisha miaka 100.
0 Comments:
Post a Comment