Toleo jipya la Nokia 3310 |
KAMPUNI ya simu za Nokia imeingia tena sokoni kwa kuishangaza dunia
baada ya kutambulisha toleo za zamani la simu yao
Nokia 3310 ambayo lilikuwa maarufu sana
mwanzoni mwa karne ya 21.
Aina hiyo ya simu kwa ukanda wa Afrika Mashariki hususani Tanzania
ilikuwa maarufu kwa jina la ‘Jeneza’ kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuhimili
mikikimikiki ikiwamo kutunza chaji.
Uzinduzi wa toleo hilo ambalo
limeboreshwa umefanyika mjini Barcelona
nchini Hispania ambako ulionyeshwa kwenye kioo kikubwa wakati wa Kongamano la
Simu za Viganjani la Dunia.
Bei yake itakapoingia sokoni ni dola 52 sawa na Shilingi Laki moja na
ishirini za Tanzania .
Wachambuzi wa masuala ya uchumi
wanasema kuingia sokoni kwa toleo hilo
kutashusha thamani ya simu za smart ambazo zimetapakaa kwa wingi duniani kwa sasa
hususani kwa nchi zinazoendelea.
Ikumbukwe Nokia wana matoleo manne ya simu zake kwenye soko zinazoanzia
euro 139 hadi 299.
Mkurugenzi Mkuu wa Nokia Rajeev Suri aliuambia mkutano huo kuwa ujio wa
toleo hilo
utawavuta wengi isivyo kawaida.
Nokia 3310 ya kwanza iliuza simu milioni 126 na kuwa ya 12 katika
historia ya mauzo ya simu za viganjani duniani.
Kongamano la Simu za Viganjani la Dunia litatia nanga Machi pili mwaka
huu huku ikitarajiwa Juni 28 hadi Julai Mosi mwaka huu kufanyika tena jijini Shanghai , China .
Toleo la kwanza la Nokia 3310 |
0 Comments:
Post a Comment