NA PENDO MICHAEL
Gazeti la Habari Leo Februari 14, 2017 kuhusu Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kukabidhi majina 97 |
SIKU
moja baada Rais John Magufuli kumwapisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na
Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga na kumtaka kusimamia kwa uadilifu
mkubwa kwa mujibu wa sheria, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amemkabidhi
majina 97 ya wanaojihusisha na biashara ya hiyo.
Hata hivyo Makonda alimtangaza mtu mmoja aitwaye Rashid Said maarufu Chidi Mapenzi akimtaka kufika Kituo cha Kikuu cha Polisi.
Makonda
alimkabidhi majina hayo bila kuyataja katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi
wa Mwalimu Julius Nyerere jana huku akisema malengo ya kuanzisha mapambano hayo
ni kuwasaidia wahanga wa dawa hizo.
Katika
siku za hivi karibuni Makonda amekuwa akilaumiwa na watu wa kada mbalimbali kwa
namna anavyoendesha kampeni kupambana na dawa za kulevya, baada ya kitendo cha
leo wadau mbalimbali wamesema huenda amepata ushauri na maoni ya namna ya
kuendesha zoezi hilo .
Kwa
upande wake Sianga ameahidi kutoa ushirikiano, na ameongeza kuwa atashughulikia
kesi zote ambazo zimekuwa zikivurugwa na mahakimu.
Wengine
waliokuwapo katika hafla hiyo ni Mchungaji George Fupe wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania , Dayosisi
ya Mashariki na Pwani, Sheikh Mkuu mkoa wa Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya
Amani Alhadi Mussa, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna Simon
Sirro.
Paul Makonda akizungumza jambo kuhusu dawa za kulevya. |
0 Comments:
Post a Comment