Mchoro wa msanii ukionyesha sayari Kepler -452b |
NA
MWANDISHI WETU
Shirika la Anga za Juu la Marekani
(NASA) leo linatarajiwa kutangaza ugunduzi "mkubwa" kuhusu mambo
yaliyomo ‘Nje ya mfumo wetu wa jua’.
Hafla ya kutangaza
ugunduzi huo itapeperushwa moja kwa moja kupitia runinga ya NASA na katika
mtandao wa shirika hilo mwendo wa saa tatu Afrika Mashariki.
Habari kuhusu
tangazo hilo pia zitachapishwa katika jarida la
kisayansi la Nature na baadaye katika Reddit.
Mwaka 2015, Dkt
Joe Michalski wa Makumbusho ya Historia ya mambo Asilia London alisema,
"Duniani, popote unapopata maji, huwa kuna uhai."
Moja ya viashiria
vya kuwepo na viumbe hai anga za juu au katika sayari nyingine ni uwepo wa
maji.
CHANZO: BBC
0 Comments:
Post a Comment