Thursday, February 9, 2017

Twitter katika wakati mgumu

SAN FRANCISCO, MAREKANI    
              
WAMILIKI wa mtandao wa kijamii wa Twitter wenye makao makuu jijini San Francisco nchini Marekani wamesema wawekezaji wa matangazo katika kampuni hilo wamekuwa wakipungua siku hadi siku.
Katika taarifa yao mapema leo wamesema ukuaji wa mapato katika kampuni hilo umekuwa ukienda taratibu tofauti na ilivyotarajiwa tangu walipoanza kupaa hewani mwaka 2013.
Wameongeza kuwa wamekuwa na upinzani mkubwa kutoka makampuni ya Snap Chat na Facebook wakipanda kwa asilimia moja hadi kufikia dola milioni 717.2
Aidha wamesema hisa za kampuni hilo zimeanguka kwa asilimia 10 hadi kufikia dola 16.81.
Mapato yatokanayo na matangazo yamekuwa yakishuka mwaka hadi mwaka hadi kufikia dola milioni 638 na kampuni hilo limeonya kwamba ukuaji wake utakuwa shida mwaka huu.
Matokeo mbalimbali yanaonyesha kuwa wateja wengi wa matangazo wamekuwa wakizipeleka dola zake katika kampuni la Facebook.
Juma lililopita Facebook limekuwa likipata mapato makubwa na kufikia dola bilioni tatu hadi sasa.

Twitter ilianzishwa Machi 21, 2006 na Jack Dorsey, Noah Glass, Biz Stone na Evan Williams

0 Comments:

Post a Comment