Kampuni linalojihusisha na kusanifu, kutengeneza,
kuendeleza na kuuza kwa wateja vifaa vya elektroniki, programu za kompyuta na
huduma za mtandao la Apple linatarajia kutoa simu iPhone 8 baadaye mwaka huu.
Hayo yanajiri ikiwa leo ni siku ya kuzaliwa
mwanzilishi wa kampuni hilo, Steve Jobs aliyefariki Oktoba 2011 huku kampuni
hilo likitarajia kuongeza aina hiyo ya simu ikiwa na maboresho zaidi ya matoleo
yaliyopita.
Kampuni hilo
limesema vioo vyenye kutumia LCD vitaendelea kubaki kwa miaka kadhaa ijayo
licha ya kuingiza teknolojia mpya ya OLED.
Toleo hilo
litajumuisha chaji isiyotumia waya, kioo chenye muundo wa OLED na kihisio cha
Three D.
Apple imekuwa ikipanda kila siku katika kuingiza
matoleo yake sokoni kutoka iPhones milioni 220 hadi 330. Jarida la Investor
limesema kuingizwa kwa iPhone 8 sokoni kutachangia mauzo kwa asilimia 30.
Mwaka 2015 Apple walitumia kiasi cha dola Bilioni
1.8 katika matangazo, ikiwa ni kiasi kikubwa ikilinganishwa na mwaka 2007
walipotumia dola Milioni 467 kutangaza ingizo la kwanza la iPhone sokoni.
Nchini Tanzania
wengi wamekuwa na matumizi makubwa ya simu za iPhone kwa sasa baadhi yao wakiona kuwa ziliwahi
kuingia mno hivyo kuendelea kuwatia umaskini kwani vipato vyao na bei za simu
hizo havilingani na baadhi wakionekana kufurahi huduma zake.
Steve Jobs alifariki akiwa na miaka 56, huku
waanzilishi wengine wa kampuni hilo
Ronald Wayne na Steve Wozniak wakiwa bado hai.
Steve Jobs enzi za uhai wake |
0 Comments:
Post a Comment