BALI, INDONESIA
Mashuhuda wa tukio wakisaidiana na waokoaji kupata manusura wa ajali hiyo. (Picha na Disaster Management Agency: Sutopo
Purwo Nugroho)
|
WATU 12 wamefariki dunia baada ya maporomoko
matatu ya ardhi yaliyoambatana na mvua kubwa kudondoka kwenye nyumba ya starehe
katika kisiwa cha Bali nchini Indonesia .
Vijiji vitatu katika wilaya ya Kintamani,
kwenye miteremko ya Mlima Batur Volcano vimeathirika huku nyumba zikiharibiwa
na vifo kutokea akiwamo mtoto wa kiume mwenye mwaka mmoja.
Ofisa wa Wakala wa Maafa na Uokoaji wa taifa hilo Indra Kalak amesema
watu kadhaa waliojeruhiwa wamekimbizwa hospitalini. Ofisa huyo ameonya juu ya wakazi wa eneo hilo wanaokaa katika
miteremko mikali huku ikitarajiwa mvua kubwa kuendelea wikiendi hii.
0 Comments:
Post a Comment