NA MWANDISHI WETU
Mkalama, Singida; Mei 2016 (Picha na Maktaba) |
BARAZA
la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida limewafukuza
kazi watumishi wake watatu na kumsimamisha kwa muda mmoja kwa tuhuma
mbalimbali, ikiwamo utoro kazini.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya hiyo James Mkwega amewataja watumishi waliokumbwa na
adhabu hiyo ni James Kidumo Moses
aliyekuwa Afisa Mifugo Msaidizi, Sera Ogoti ambaye ni Afisa Muuguzi na Selemani Ntunga aliyekuwa Fundi Sanifu wa Maabara.
Mkwega
amekiambia Kikao cha Baraza la Madiwani Mjini Nduguti kuwa watumishi hao watatu
wamefukuzwa kazi kutokana na kushindwa kuonekana kwenye vituo vyao vya kazi
bila taarifa yoyote kwa miezi miwili kinyume cha sheria za Utumishi wa Umma.
Pia Halmashauri
hiyo imemsimamisha kazi Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF awamu tatu
katika Wilaya hiyo, Athuman Dule kutokana na tuhuma za kusajili kaya 28
zisizokuwa na sifa za kuingizwa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya masikini ili
kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.
0 Comments:
Post a Comment