PHNOM PENH,
CAMBODIA
Gereji ya Vifaa vya Kijeshi iliyojengwa kwa msaada wa
Serikali ya China imezinduliwa nchini Cambodia.Ujenzi wa gereji hiyo ambayo
itatumika kurekebisha vifaa vya kijeshi ilianza kujengwa mwaka 2015.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi wa Cambodia
Jenerali Tea Banh akiwa na Balozi wa China nchini humo Xiong Bo wamezindua
gereji hiyo katika Kikosi magari ya kijeshi Namba 99 kilichopo mjini mkuu Phnom
Penh. Taarifa kutoka nchini humo zinasema gereji hiyo yenye teknolojia mpya ina
ukubwa mita za mraba 500 ambayo itakuwa muhimu kwa Jeshi la Ulinzi la nchini
hiyo. Uhusiano wa Cambodia na China uliimarika baada ya kumalizika kwa vita ya
Cambodia na Vietnam mwaka 1991.
Wakati huo huo takwimu zinaonyesha kubwa idadi kuwa ya
Wachina imekuwa ikiongezeka katika nchi ya Ukraine kutokana na urahisi wa
kupata viza na uhusiano wake na taifa hilo la Ulaya. Takwimu hizo za Ukraine
zimeonyesha raia wa China 20,555 wamezuru nchi hiyo mwaka jana ikilinganishwa
na 13,602 mwaka 2015. Tangu Juni 2016 Ukraine ilianza kutoa viza ya siku 15 kwa
wafanyabiashara na watalii raia wa China waliokuwa wakifika nchini humo kwa
kutumia uwanja wa ndege wa Kiev Boryspil. Miezi minne baadaye Ukraine iliweza
kutunga sera ya kuongeza matumizi ya viza hiyo hadi mji wa Odessa ulio kusini
mwa Bahari Nyeusi.
0 Comments:
Post a Comment