Kwa mujibu wa Forbes inasema tajiri namba moja nchini Tanzania Mohammed Dewji (49) maarufu Mo katika nafasi za mabilionea mwaka 2025 ni 1588.
Mo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa METL amekuwa akifanya
kazi Afrika Mashariki na Kati katika nchi za Kenya, Ethiopia, Uganda na
Tanzania.
Hadi tarehe 8 Machi 2025 Mo ametajwa kuwa na utajiri wa Dola za Kimarekani 2.2 bilioni ikimweka katika nafasi hiyo; Utajiri huo umepanda kutoka Dola la Kimarekani 1.8 bilioni Januari 2024 ukimweka wakati huo katika nafasi ya 12 barani Afrika.
Mnamo mwaka 2016 ndiye Mfanyabiashara pekee nchini Tanzania
alisaini Giving Pledge akitoa ahadi ya kujitolea walau nusu ya utajiri wake kwa
ajili ya wenye mahitaji (philanthropic causes).
Kama ilivyo kwa wafanyabiashara wengine, ushindani ni suala
la muhimu; Mo ameendelea kutoa ushindani kwa makampuni kama Coca Cola kwa
kuzalisha kinywaji kipya cha Mo Cola.
Mpaka sasa Mo Dewji ndiye mtanzania pekee aliyepo kwenye
orodha ya mabilionea wa dunia
Kwa mujibu wa Forbes, Elon Musk, Mark Zuckeberg na Jeff Bezos
wanashika nafasi za juu za mabilionea duniani.
Wakati huo huo Forbes imemtaja Rais wa Shiriksho la Soka
Barani Afrika Patrick Motsepe (63) kuwa ni Bilionea wa 1173.
Utajiri wa Motsepe wa Dola za Kimarekani 3 bilioni unafanya
katika taifa lake la Afrika Kusini kushika nafasi ya nne akizidiwa na Koos
Becker ambaye duniani anashika nafasi ya 1049, Nick Oppenheimmer & family
nafasi ya 254 na tajiri namba moja nchini Afrika Kusini Johann Rupert & family
anayeshika nafasi ya 164.
Aidha ni matajiri sita pekee kutoka Afrika Kusini ambao wapo
katika orodha ya mabilionea wa dunia wa Forbes.
Credit to: Jabir Johnson/JAIZMELA/Forbes.
0 Comments:
Post a Comment