Thursday, February 20, 2020

MAKTBA YA JAIZMELA: Papa Martin V ni nani?


Februari 20, 1431 alifariki dunia kiongozi wa juu wa Kanisa Katoliki Papa Martin V. 

Jina lake halisi ni Oddo au Oddone  au Colonna. Alizaliwa katika viunga vya Genazzano nchini Italia ambako ilikuwa mojawapo ya sehemu katika eneo la umiliki wa Papa. 

Alikamata wadhifa huo kutoka mwaka 1417 hadi alipofariki dunia. Alifariki dunia kwa kiharusi akiwa na umri wa miaka 62. 

Papa Martin V ni miongoni mwa mapapa wa kanisa hilo ambaye alichaguliwa katika kipindi mwisho cha mpasuko katika Kanisa Katoliki kilicholikumba kanisa hilo kati ya mwaka 1378 hadi 1417. 

Kipindi hicho kila mmoja alijitangaza kuwa Papa wa kanisa hilo. 

Akiwa katika wadhifa huo alikutana na magumu kutokana na kwamba aliingia katika kipindi ambacho kanisa lilikuwa limevurugika hivyo alikuwa na kazi kubwa ya kulirudisha katika mstari wake. 

Alipeleka mapendekezo yake ya namna ya kurudisha kanisa hilo katika mstari mbele ya Baraza la Constance ambalo lilikubali mapendekezo yake kutawala ardhi na miji iliyokuwa ikimilikiwa na kanisa. 

Katika hili alipendelea zaidi iitumike njia ya kidplomasia badala ya nguvu. 

Baada ya kukubalika kwa hilo alizuia kabisa suala la Papa kupingwa katika maamuzi atakayokuwa akiyafanya hususani yanayohusu imani. 

Wakati akikalia kiti cha upapa wa Kanisa Katoliki biashara ya utumwa ilikuwa imeshamiri hivyo barani Ulaya ilikuwa imeanza kushuka. 

Hivyo Kanisa Katoliki lilitangaza kuwa ni dhambi kuwafanya Wakristo kuwa Watumwa. Licha ya kutangaza hivyo haikuwa kazi rahisi kuondoa safari na misafara mbalimbali ya watumwa hao. 

Tangazo hilo la kanisa liliacha maswali mengi kama wakristo ambao ni nje ya Ulaya watakuwa wameruhusiwa au la. 

Kwa mujibu wa Burton, alisema Martin aliidhinisha vita takatifu barani Afrika mnamo mwaka 1418 na kwamba Papa Eugene IV ambaye alipokea mikoba ya Martin V  aliwakata Wareno kuchukua Watumwa wa kutoka barani Afrika. 

Mnamo Machi 1425 kulitolewa kitisho kikali kwa Wakristo waliokuwa wakifanya biashara ya Utumwa na Wayahudi kutakiwa kuvaa kitambaa mabacho kitwatambulisha kutoka na tabia hiyo mbaya. 

Juni 1425 Papa Martin V aliwalaani wale wote waliokuwa wakiwauza watumwa wa Kikristo kwa Waislamu. Misafara ya Watumwa waliokuwa waamini wa dini ya Kikristo haikuweza kusitishwa  kwenda kwa wale ambao hawakuwa Wakristo.  

Kwa mujibu wa Koschorke, alisema Papa Martin V alikuwa aikunga mkono utafutaji wa makoloni ili kupanua zaidi dola la Rumi. 

Davidson (1961) alikaririwa akisema kuwa kuingilia kati suala la Utumwa kulikofanywa na Papa Martin V haikuwa dawa kamili ya kuuzua utumwa bali ilikuwa ni kuongeza hofu ya matumizi na vitendo vya kinyama kwa watumwa.

Mnamo mwaka 1281 wakati jina la Papa wa Pili wa Kanisa Katoliki alipochagua kutumia Martin kulitokea mkanganyiko wa jina hilo kuwa ni Mapapa wangapi waliowahi kutumia jina hilo hapo kabla. 

Iliaminika kuwa walikuwa watatu  hivyo Papa wa mwaka 1281 angekuwa Martini IV. 

Lakini kwa uhalisi wake, waliokuwa wanaamini kuwa kulikuwa na Martin II na Martin III walitajwa kuwa walikuwa wakitumia Marinus I na Marinus II. 

Mara kadhaa baadaye walichukuliwa kuwa Martin I, Martin II na Martin III. Hivyo ilisaidia waliofuata baada ya hao kutumia Martin IV na V. Hata hivyo Martin IV na Martin V hao ndio wa kwanza na wa pili.

Akiwa Rome, makazi ya Papa Martin V yalianzia Lateran hadi Santa Maria Maggiore  na kutoka mwaka 1424 alikwenda Basilica ya Santi Apostoli karibu na Pallazo. Kuna wakati pia alikuwa akikaa katika miji waliopo ndugu zake kwa muda huko Latium kwenye vitongoji vya (Tivoli, Vicovaro, Marino na Gallicano.

Kabla ya  Rome Wafaransa walitoa mji Avignon, Ufaransa kutoka mwaka 1309 hadi 1377 uwe makazi ya Papa.  Papa Martin alizaliwa kati ya  Januari 26 na Februari 20, 1369

Mwaka 2017 kanisa Katoliki liliadhimisha miaka 600 ya Papa Martin V tangu aliposhika madaraka hayo Novemba 14, 1417 hadi kifo chake Februari 20, 1431.


0 Comments:

Post a Comment