Saturday, February 29, 2020

Unaikumbuka siku Middlesbrough ilipowashangaza Bolton ya Jay Jay Okocha?

Februari 29, 2004 ilikuwa siku njema kwa klabu ya Middlesbrough ya England pale ilipovunja vitasa vya Bolton katika mchezo wa fainali ya Kombe la Ligi. 

Mabao mawili ya haraka yalitosha kuipa taji Middlesbrough. Na hilo lilikuwa taji lake la kwanza kubwa katika historia ya klabu hiyo. 

Klabu ya Middlesbrough ilianzishwa mnamo mwaka 1876. 

Miaka miwili kabla Middlesbrough walikaribia kuchukua taji la FA na Kombe la Ligi mnamo mwaka 1997 walipofika fainali katika michuano hiyo. 

Mnamo mwaka 1998 Middlesbrough walirudi katika fainali ya Kombe la Ligi lakini walishindwa kuchukua taji hilo. 

Walipofika fainali ya Kombe la Ligi  kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1997 walipambana na Leicester City ambao walitwaa baa da ya mchezo wa marudiano. 

Wangeweza kuchukua lakini ndio hivyo.

Bolton walikuwa na historia ya kutwaa taji la FA mara nne wakifanya hivyo 1923, 1926, 1929 na 1958. 

Bolton walifika fainali ikiwa ni baada ya kushindwa mbele ya Liverpool kwa mabao 2-1 dhidi ya Liverpool mnamo mwaka 1995.

Miamba hiyo ilikutana katika dimba la Millenium jijini Cardiff mbele ya watazamaji 72,634  ambao walikosa kuliona bao la kwanza siku hiyo. 

Ikiwa ni dakika ya pili ya mchezo wakiwa bado wanajiweka sawa katika viti vyao vya kukalia kiungo wa Middlesbrough Boudewijn Zenden alifumua mkwaju mkali katika lango la Bolton ambao ulimkuta mshambuliaji wao Joseph Desire na kuipa uongozi Middlesbrough.

Dakika tano baadaye Zenden aliipa uongozi Middlesbrough kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa kati wa Bolton Emerson Thome kumchezea rafu Job ndani ya eneo la hatari. 

Bolton walijaribu kuliandama lango la Bolton ambapo juhudi zao zilitaka kuzaa matunda katika dakika ya 21 ya mchezo kupitia kwa nyota wao Kevin Davies  lakini mlinda mlango wa Middlesbrough Marl Schwarzer aliokoa mchomo huo hivyo mchezo ukamalizika kwa mabao 2-1. 

Kwa wakati huo bao la mapema lilifungwa na Job na kuwa bao la mapema katika historia ya Kombe la Ligi kwa wakati huo.

Rekodi hiyo ilikuja kuvunjwa na nyota wa Loverpool John Riise aliyefungwa kwenye michuano hiyo katika dakika ya kwanza ya mchezo mwaka uliofuata.

0 Comments:

Post a Comment