Saturday, February 1, 2020

Ufahamu mwezi Februari

Februari ni mwezi wa pili wa mwaka katika kalenda ya Julian na ile ya Gregori ukiwa na siku 28 katika mwaka mfupi au siku 29 kwa mwaka mrefu. 

Februari ndio mwezi wa kwanza kati ya mitano wenye siku chache zilizo chini ya siku 31 mingine ni Aprili, Juni, Septemba na Novemba. 

Pia Februari ndio mwezi pekee ambao una siku chini ya 30 miezi mingine saba ina siku 31. 

Mwaka 2020, Februari ina siku 29. Mwezi huu uliitwa Februarius na Warumi ambao walichukua mzizi wa kilatini Februum ikiwa na maana ya utakaso. 

Ibada hiyo ya kujitakasa kwa mujibu wa kalenda ya zamani ya Kirumi ilikuwa ikifanyika kila Februari 15 wakati mwezi unapojaa wote. 

Ikumbukwe Januari na Februari ndio miezi miwili ya mwisho kuongezwa katika kalenda ya Kirumi. Hiii ilitokana na Warumi walikuwa wakiichukulia miezi hii kuwa ni kipindi cha baridi na giza. 

Inaelezwa kuwa Mtawala wa Rumi wakati huo Numa Pompilius alifanya hivyo mwaka 713 K.K Hadi mwaka 450 Februari ulikuwa ni mwezi wa mwisho katika kalenda ya Kirumi kabla ya Decemvirs alipobadilisha na kuuweka kuwa ni mwezi wa pili. 

Kuna wakati Februari ilikuwa na siku 23, 24 na 27.

0 Comments:

Post a Comment