Monday, February 17, 2020

Unaikumbuka rekodi ya Real Madrid ya kutopteza mechi 121?

Februari 17, 1957 miamba ya soka nchini Hispania Real Madrid iliweka rekodi ya kutofungwa mechi 121 katika uwanja wake wa nyumbani pale ilizabua Deportivo de La Coruña ikiwa ni mfululizo wa mechi za La Liga. 

Mchezo huo ulikuwa wa kwanza wakitoka ugenini kupoteza dhidi ya Atletico Madrid majuma mawili kabla. 

Los Blancos waliichapa Deportivo kwa bao 1-0 kupitia kwa nyota wake Enrico Mateos. Bao hilo lilitinga nyavuni katika dakika ya 25. 

Mechi tatu zilizobaki za hapo Santiago Bernabeu Los Blancos ilishinda na kutwaa taji la La Liga. Kinachostaajabisha zaidi ni pale Real Madrid ilipoendelea kutetea rekodi hiyo kwa miaka minane mingine ikifikisha mechi 121. 

Katika miaka hiyo miaka hiyo minane; Los Blancos ilitwaa mataji sita ya La Liga. Katika mechi hizo, sare zilikuwa nane pekee na 113 ulikuwa ni ushindi. 

Mchezo wa mwisho kufanya hivyo ilikuwa ni February 21, 1965 waliposhinda mabao 6-1 dhidi ya Real Betis lakini Machi 7 walipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Atletico Madrid.

0 Comments:

Post a Comment