February 11, 2003 mshambuliaji wa zamani wa Ivory Coast Didier Drogba alifunga bao lake la kwanza tangu alipoingia kuhudumu na miamba hiyo.
Bao hilo alilifunga katika mchezo dhidi ya 'Simba Wasioshindika' timu ya Taifa ya Cameroon ambao 'Tembo wa Afrika' waliibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Hadi sasa Drogba anasalia kuwa mfungaji bora wa zama zote wa taifa hilo akifunga mabao 65 katika mechi 104 alihudumu na Tembo wa Afrika.
Aliitwa katika kikosi cha Ivory Coast akiwa na umri wa miaka 24; mechi hiyo ilikuwa ya kuwania kufuzu kucheza Mataifa ya Afrika mwaka 2004 yaliyofanyika nchini Tunisia.
Katika mchezo wa kwanza walitoka sare tasa dhidi ya Afrika Kusini na mchezo uliofuata ulikuwa ya kirafiki dhidi ya Cameroon ambayo alipata fursa ya kufunga bao lake la kwanza.
Mbele ya watazamaji 3,000 katika dimba la Gaston-Petit Ivory Coast walipata uongozi katika dakika ya 37 ya mchezo kupitia kiungo wao Tchiressoua.
Dakika nane baadaye Drogba alifunga bao lake la kwanza na kuipa uongozi Ivory wa mabao 2-0 kabla ya mapumziko.
Katika dakika ya 63 Drogba alitolewa nje; alikuwa Bonaventure Kalou alipigilia msumari wa tatu kwa mkwaju wa penati uliowapa ushindi wa mabao 3-0.
Mwaka ule ule , Drogba alifunga mabao mengine matatu, licha ya Ivory Coast kushindwa kufuzu AFCON.
Drogba alibebeshwa majukumu ya kuiongoza Ivory Coast katika nafasi ya nahodha wa kikosi cha Tembo wa Afrika.
Alitajwa kuwa mchezo bora wa mwaka wa Afrika mara mbili mnamo mwaka 2006 na 2009.
0 Comments:
Post a Comment