Saturday, February 29, 2020

Dkt. Ndugulile: Nchi iko salama dhidi ya Virusi vya Covid-19

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza jambo katika mahafali ya kidato cha sita katika Shule ya Mt. Maria Goreth mjini Moshi Februari 29, 2020. (Picha na Jabir Johnson)


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulileamesema nchi ya Tanzania iko salama dhidi ya maambukizi ambayo yanatikisa dunia kwa sasa ya virusi vya Covid-19.

Akizungumza katika mahafali ya 16 ya kidato cha sita ya Shule ya Mt. Maria Goreth mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro leo Dkt. Ndugulile amesema hali ya maambukizi imeendelea kuibua hofu kwa mataifa mbalimbali lakini nchini Tanzania hali ni shwari.

“Tanzania tuko salama dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona ambayo vimeanzia China, tunaendelea kuimarisha mipaka, viwanja vya ndege kwa kuweka mifumo ya kuwaangalia wageni kutoka mataifa mbalimbali wanaoingia Tanzania,” amesema Dkt. Ndugulile.

Hata hivyo Dkt. Ndugulile amesema wameenda kuimarisha hali ya usalama katika visiwa vya Zanzibar ambako Waitaliano wengi wanatiririka huko kila wakati.

0 Comments:

Post a Comment