Februari 1, 2014 alifariki dunia mwanasoka wa zamani na Kocha wa Hispania Luis Aragones Suarez.
Aragones alifariki dunia saa 12:15 katika hospitali ya CEMTRO jijini Madrid kwa maradhi ya kansa ya damu.
Shirikisho la Soka nchini Hispania lilitoa taarifa yake kuwa ni huzuni na majonzi kwa mtu ambaye alikuwa kocha tangu mwanzo wa kipindi cha mwangaza wa soka nchini humo na dunia kwa ujumla.
Kocha Diego Simeone ambaye ni kocha wa Atletico Madrid alisema,"Ningependa kupeleka ujumbe wangu muhimu kwa familia, kuwa kila mmoja wetu katika Atletico ameumizwa na kumpoteza muhimu katika klabu na soka la Hispania. Aliyechukua mikoba ya Aragones Vicente Del Bosque naye alipata wasaa wa kutoa neno, "
Tumeshtushwa na taarifa za kusikitisha, Luis alikuwa baba wa mafanikio kwa timu ya taifa. Sisi sote katika ukumbi huu, siku zote tutaendelea kumkumbuka katika kumbukumbu zetu."
Aragones alizikwa Februari 2, 2014 jijini Madrid katika maziko ambayo yalihudhuriwa na wachezaji waliowahi kuwa mikononi mwake wakiwamo Carles Puyol, Cesc Fàbregas, Andrés Iniesta na Xavi.
Aragones alizikwa katika makaburi ya La Paz huko Alcobendas.
Katika fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya mwaka 2014 klabu ya Atletico Madrid walivaa mashati yaliandikwa jina la Aragones. Jina hilo liliandikwa kwa rangi ya dhahabu ndani ya upindo wa ndani wa kola.
Klabu ya Atletico Madrid ilitoa heshima zake kwa Luis Aragones katika msimu wa 2019-2020 pale ilipompa kadi ya uanachama wa klabu hiyo. Aidha sanamu ya kuenzi mchango wake katika soka imewekwa nje ya uwanja wa Wanda Metropolitan ambao ni uwanja wa nyumbani wa Atletico Madrid.
Aragones alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 75. Alizaliwa Julai 28, 1938.
Katika maisha yake ya soka alitumikia muda mrefu katika klabu ya Atletico Madrid kuliko klabu nyingine nchini Hispania licha ya kwamba aliwahi kuzitumikia klabu nyingine nchini humo ikiwamo Real Betis.
Alikuwa mchezaji muhimu ambaye baadaye alikuja kuwa kocha baada ya kustaafu mapema miaka ya 1970. Kati ya mwaka 1964 hadi 1974 alicheza mechi 265 akiwa na Atletico na kufunga mabao 172.
Katika timu ya taifa alicheza mara 11 na kufumania nyavu mara tatu tu.
Akiwa kocha aliipa mataji mara nne ya La Liga, aliifikisha fainali ya Kombe la Ulaya. Mbali na kuinoa Atletico aliwahi pia kuzifundisha timu nyingine saba nchini Hispania na pia timu ya taifa ya Hispania aliyoipa taji la pili la Ulaya mwaka 2008.
Aliinoa Hispania kuanzia mwaka 2004. Pia aliwahi kuinoa klabu ya Fenerbahce ya Uturuki ikiwa ni mara yake ya kwanza kufundisha nje ya Hispania.
Aragones alianza maisha yake ya soka mnamo mwaka 1957 akiwa na CD Getafe na baadaye Real Madrid ilimuona.
Akiwa na Los Blancos hakufanikiwa kupata nafasi katika timu ya wakubwa hivyo hakucheza hapo, isipokuwa alitolewa kwa mkopo katika klabu mbalimbali ikiwamo Recreativo de Huelva na Hercules.
Mnamo mwaka 1960 alijiunga na Real Oviedo kwa mwaka mmoja na baada ya hapo kati ya mwaka 1961 na 1964 Real Betis ilikuwa naye ambako alicheza mechi 86 alifunga mabao 33.

0 Comments:
Post a Comment