Wednesday, February 12, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Immanuel Kant ni nani?

Februari 12, 1804 alifariki dunia mwanafalsafa wa Ujerumani Immanuel Kant. 

Alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 80. Hakuoa aliishi na mtumishi wa nyumbani tu hadi kifo chake. Anahesabiwa kati ya wanafalsafa muhimu zaidi wa zama za mwangaza.  

Mwanafalsafa huyo alijikita hasa katika masuala ya akili akisema "Sapere aude!" akimaanisha : "Usiogope kutafakari mwenyewe". 

Aliona ni muhimu ya kwamba kila mtu atumie akili yake mwenyewe badala ya kutegemea mawazo ya watu wengine. 

Mawazo na mafundisho yote yanapaswa kupitia kwenye uhakiki wa akili.

Kwa njia hii alitafsiri mwelekeo wa zama za mwangaza na wengi wanamwona kuwa alikamilisha jitihada za mwangaza. 

Kant aliandika: "Mwangaza inamaanisha kuondoka kwa binadamu kutoka uchanga wake uliosababisha mwenyewe. 

Uchanga unamaanisha kutotumia akili bila mwongozo wa mwingine. Uchanga huu husababishwa na mtu mwenyewe si kwa sababu ya uhaba wa akili lakini kwa sababu ya uhaba wa nia na hofu ya kutumia akili bila mwongozo wa mwingine."

Kaburi lake lipo kando la kanisa kuu la Königsberg limetunzwa hadi sasa baada ya kufukuzwa kwa Wajerumani na kuwa sehemu ya Urusi. 

Hali ya kiafya ya mwanafalsafa huyu ilianza kwenda vibaya na hatimaye kufariki dunia akitamka maneno ya mwisho 'Es ist gut' akimaanisha 'Ni vizuri'. 

Kazi zake nyingine za mwishoni zilichapishwa kama 'Opus Postumum.' 

Baada ya kifo chake alizikwa na wakati ambao mwili wake ulipohamishwa katika eneo jipya la maziko fuvu lake lilipimwa na kuonekana kuwa lilikuwa kubwa kuliko wastani wa mwanaume wa Kijerumani. 

Lilionekana kubwa na pana hivyo wengi walirejea mafundisho yake hususani mwishoni mwa karne ya 18 na mwanzoni mwanzoni mwa karne ya 19.

Kant alizaliwa Aprili 22, 1724 katika mji wa Königsberg,  ambao kwa sasa ni Kaliningrad nchini Russia wakati huo ukiwa ni katika Himaya ya Prussia.

Kant alikuwa mtoto wa fundi. Mamake alimsomesha kweye shule ya sekondari akaendelea kusoma theolojia, falsafa, sayansi, fizikia na hisabati. 

Tasnifu (thesis) yake ya kwanza haikupokelewa na profesa wake mwaka 1746 hivyo alifanya kazi ya mwalimu kwenye nyumba ya matajiri na makabaila mbalimbali kwenye mazingira ya Königsberg.
Mnamo mwaka 1754 alirudi kwenye chuo kikuu akamaliza masomo yake. Tangu 1755 alikuwa mwalimu na tangu 1870 profesa kamili kwenye chuo kikuu cha Königsberg.

 Kazi muhimu za Kant zilijikita katika Maadili, Dini, Sheria, Mazingira, Unajimu na Historia zikiwamo The Universal Natural History (1755), the Critique of Practical Reason (1788), the Metaphysics of Morals (1797), na the Critique of Judgment (1790).

Kant alijiuliza maswali manne: 1. Ninaweza kujua nini? 2. Ninatakiwa kufanya nini? 3. Ninaweza kutumaini nini? 4. Binadamu ni nini ?

Mwaka 1871 alitoa kitabu cha "uhakiki wa akili tupu". Humo aliuliza swali je akili inaweza kujua nini bila maarifa.

Halafu alitazama mipaka ya akili. Akili inataka kuendelea lakini inagonga mipaka. Maswali kama: Je kuna roho ndani ya mtu isiyokufa? Kuna Mungu? Dunia haina mipaka? yanahusu mambo ambayo akili haiwezi kujibu kwa uhakika. Hakuna uthibitisho kwa namna ya uthibitisho wa kisayansi.

"Uhakiki wa akili tendaji" ni kitabu cha pili kinachoendeleza kile cha kwanza. Akili tendaji ni matumizi ya akili kwa maadili ya kutenda yale ambayo ni mema na sahihi.

0 Comments:

Post a Comment