Kikosi cha Polisi Tanzania dhidi ya Yanga Februari 18, 2020 katika dimba la Ushirika, Moshi |
Kikosi cha Yanga dhidi ya Polisi Tanzania Februari 18, 2020 katika dimba la Ushirika, Moshi |
Yanga SC imeendelea kusuasua baada ya kulazimishwa sare ya tatu mfululizo katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara kufuatia kufungana 1-1 na wenyeji, Polisi Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Ikumbukwe, Yanga SC ilitoa sare za 0-0 na Mbeya City na 1-1 na Tanzania Prisons, zote za Mbeya kwenye mechi zake mbili zilizopita Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Na sare ya leo inamaanisha wameshindwa kuifunga Polisi msimu huu, kwani hata mechi ya kwanza walitoka sare ya 3-3 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam tena Yanga wakitoka nyuma 3-0 kipindi cha kwanza.
Katika mchezo wa leo, Yanga SC ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata leo, mfungaji Tariq Seif Kiakala dakika ya 41 akimalizia pasi ya kiungo Mghana, Benard Morison.
Lakini Polisi Tanzania wakasawazisha bao hilo dakika ya 67 likifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Matheo Anthony Simon kwa kichwa akimalizia krosi ya Suxtus Sabilo, ambalo hata hivyo lilikataliwa.
Refa Abel William alimfuata msaidizi wake namba moja, Martin Mwaliaje kushauriana naye na wakalikataa bao hilo.
Lakini Polisi Tanzania hawakukata tamaa – na kwa kutumia makosa ya aina ile ile ya safu ya ulinzi ya Yanga, wakafanikiwa kupata bao lingine dakika tatu baadaye, mfungaji Sixtus Sabilo akimalizia pasi ya Marcel Kaheza dakika ya 71.
Kikosi cha Polisi Tanzania kilikuwa; Mohamed Yussuf, William Lucian, Yassin Mustapha, Iddy Mobby, Mohammed Kassim, Pato Ngonyani, Jimmy Shoji, Baraka Majogoro/Mohamed Mkopi dk62, Matheo Anthony, Marcel Kaheza na Sixtus Sabilo.
Yanga SC; Farouk Shikharo, Juma Abdul, Jaffar Mohamed, Kelvin Yondan, Lamine Moro, Pappy Kabamba Tshishimbi, Ditram Nchimbi, Haruna Niyonzima/Abdulaziz Makame dk85, Tariq Seif/Yikpe Gislain dk64, Mapinduzi Balama/Deus Kaseke dk78 na Benard Morrison.
0 Comments:
Post a Comment