Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuizabua Kagera Sugar 1-0 usiku wa jana Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 59 katika mchezo wa 23, ikitanua uongozi wake kwa pointi 15 zaidi ya Azam FC wanaofuatia ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi na leo watamenyana na Ndanda FC mjini Mtwara.
Mchezo huo uliochezeshwa na refa Martin Saanya wa Morogoro aliyesaidiwa na Arnold Bugado wa Tanga na Rashid Zongo wa Iringa.
Bao pekee la Simba SC limefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Meddie Kagere kwa penalti dakika ya 60 baada ya John Bocco kuchezewa rafu na mlinda mlango Tinoco.
CHANZO: Bin Zubeiry
0 Comments:
Post a Comment