Alhamisi ya Februari 26, 2015 alifariki mchezaji wa kikapu na wa kwanza Mmarekani Mweusi kucheza Ligi Kuu ya Kikapu nchini Marekani Earl Lloyd.
Nyota huyo alifariki akiwa na umri wa miaka 86.
Lloyd aliweka rekodi hiyo katika historia ya NBA mnamo mwaka 1950 akiwa na Washington Capitals ikiwa ni kabla ya marafiki wenzake weusi Sweetwater Clifton na Chuck Cooper nao kuweka rekodi hiyo.
Rais wa West Virginia wakati huo Brian Hemphill alisema familia nzima ya West Virginia inaomboleza kuondokewa na nyota huyo ambaye alikuwa mshinda ndani na nje ya Uwanja.
Hemphill alikaririwa akisema wakati Llyod alipokuwa akiingia mwaka ule wa 1950 alifungua njia ya usawa katika taifa la Marekani.
Lloyd aliisaidia Sycrause Nationals kutwaa taji la NBA mwaka 1955 akiungana na mchezaji mwingine mweusi Jim Tucker kucheza.
Lloyd alikuwa na kimo cha futi 6 na inchi tano akiwa na wastani wa kufunga pointi 8.4 na wastani wa rebaundi 6.4 na mechi akali ya 560.
Aliukosa msimu 1951 na 1952 kutokana na kwamba wakati huo alikuwa akilitumikia jeshi la Marekani.
Katika medani ya kikapu kuna wakti aliwahi kumsaidia kutafuta kikosi kocha Bailey Howell hapo ndipo alipopata fursa ya kubaini vipaji vya nyota Willis Reed, Earl Monroe, Ray Scott na Wally Jones.
Pia nyota huo wa kikapu aliwahi kuwa kocha wa Detroit mwaka 1971 -1972 na pia alisimamia kikosi cha Pistons kwa mechi tisa za kwanza za msimu wa 1972-1973 na baada ya hapo alitimuliwa kutokana na matokeo mabaya akiwa na rekodi ya kushinda mechi 22 kati ya 55.
Mnamo mwaka 2003 aliingizwa katika Jumba la Wakongwe wa Kikapu kutokana na mchango wake katika mchezo huo.
Alizaliwa Alexandria huko Virginia lakini alikuwa akiishi Crossville huko Tennessee.
Lloyd alizaliwa Aprili 3, 1928 kwa wazazi Theodore Llyod Sr. na Daisy Lloyd.
Baba yake alikuwa mfanyakazi katika kiwanda cha makaa ya mawe na mama yake alikuwa ni mama wa nyumbani. Alipata elimu yake kwa taabu kutokana na ubaguzi wa rangi uliokuwa umeshamiri nchini Marekani.
Hata hivyo alipita vigingi vyote na kufika high school ambako alitajwa katika kikosi cha All-Soutj Atlantic Conference mara tatu pia mara mbili aliitwa katika kikosi cha kikapu cha All-State Virginia.
Kuna wakati Lloyd aliwashukuru familia yake na walimu waliomsaidia kupita katika vipindi vigumu wakati wa masomo yake hadi kufikia mafanikio hayo.
0 Comments:
Post a Comment