Monday, February 17, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: José López Portillo ni nani?

Februari 17, 2004 alifariki dunia mwanasiasa, mwanasheria na Rais wa zamani wa Mexico José Guillermo Abel López Portillo y Pacheco. 

Mwanasiasa huyo alihudumu katika wadhifa wa juu wa taifa hilo kutoka mwaka 1976 hadi 1982 hivyo kuweka rekodi ya kuwa Rais wa 51 wa Mexico.  

López Portillo kama ambavyo alikuwa akifahamika na wengi nchini humo ndiye pekee katika zama za sasa katika historia ya Mexico kuchaguliwa pasipo kupingwa. 

Alianza kujihusisha na siasa tangu mwaka 1959. 

Aliingia madarakani kwa tiketi ya Chama cha PRI katika uchaguzi wa mwaka 1976. 

Alifariki dunia Mexico City akiwa na umri wa miaka 83 kutokana na maradhi ya kupumua na kichomi katika mapafu. 

Alizikwa katika makaburi ya kijeshi ya Pantheon Federal. 

Enzi za uhai wake alioa mara mbili mkewe wa kwanza Carmen Romano ambaye waliachana mara baada ya kumaliza urais. 

Mnamo mwaka 1995 alimuoa mpenzi wake wa siku nyingi Mwigizaji Sasha Montenegro. 

Mwigizaji huyo alimzaliwa watoto wawili ambao ni Nabila na Alejandro ambaye naye pia walikuja kuachana. 

López Portillo ni kaka wa mwandishi wa riwaya nchini Mexico ambaye alifariki dunia Mei 8, 2006 aliyefahamika kwa jina la Margarita López Portillo. 

Wakati anachukua wadhifa huo López Portillo aliikuta Mexico ikiwa mdororo wa uchumi. 

Hivyo alipambana kuuboresha uchumi wa taifa hilo kwa kugundua hazina ya mafuta ambayo yangeongeza mapato. 

Aligundua hazina hiyo huko Vercruz na Tabasco ambapo kampuni kubwa la Mafuta nchini humo Pemex lilifanya kazi hiyo. 

Sera zake za nje ilikuwa ni kutafuta soko la mafuta ambapo mwaka 1980 Mexico iliingia ubia na Venezuela kuwa na viwango sawa katika uuzaji wa mafuta hususani katika Amerika ya Kati na Carribean. 

Kwa muda mfupi alifanikiwa kuuinua uchumi wa Mexico lakini wakati anaondoka madaraka uchumi ulishuka na kuiacha Mexico ikiwa katika hali mbaya kiuchumi iliyosababisha deni kuwa kubwa. 

Wakosoaji wake wakubwa walisema enzi za utawala wake rushwa ilitanua ndimi zake na pia aliweka ndugu, jamaa na marafiki zake katika nafasi mbalimbali serikalini. 

Alipoondoka madarakani nafasi yake ilichukuliwa na Miguel de la Madrid ambaye washirika wa karibu wa López Portillo walikamatwa na kusekwa jela kwa makosa mbalimbali. 

Licha ya kuhusika kwake katika kuangusha uchumi wa taifa hilo na kukithiri kwa rushwa lakini  López Portillo hajawahi kupandishwa kizimbani kwa mashtaka yoyote. 

López Portillo  alizaliwa kwa wazazi José López Portillo y Weber (1888–1974),  ambaye alikuwa mhandisi, mwanahistoria, mtafiti na mwanataaluma na mama yake Refugio Pacheco y Villa-Gordoa. 

Alisoma masomo ya sheria  katika Chuo Kikuu cha Mexico (UNAM) kabla kujiingiza katika siasa.

0 Comments:

Post a Comment