Februari 28, 1963 alifariki dunia Rais wa Kwanza wa kuchaguliwa wa India Rajendra Prasad. Mwanasiasa huyo ambaye alisomea sheria na sayansi ya siasa alishikia wadhifa huo kutoka mwaka 1950 hadi 1962. Prasad alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 78 huko Patna.
Hali yake ya afya ilianza kuzorota mnamo mwaka 1960 alipopatwa na shambulio la moyo. Alianza kupatiwa matibabu na madatari bingwa wa nchini India akiwamo rafiki yake Dkt. Bidhan Chandra Roy kwa wakati huo alikuwa Waziri katika Jimbo la West Bengal.
Mnamo Machi 7, 1961 alianza kunyong’onyea zaidi akiwa na umri wa miaka 74 baada ya kupatwa kiharusi katika ubongo, wakati huo alikuwa bado katika Ofisi ya Waziri wa Mambo Ndani wa India. Wakati akiwa katika wadhifa huo ambao kwa mujibu wa kikatiba ya India hakuwa na nguvu kubwa sana serikali kama ilivyokuwa kwa Waziri Mkuu Jawaharlal Nehru. Mnamo mwaka 1916 alijiunga na Mahakama kuu ya Bihar na Odisha.
Mnamo mwaka 1917 aliteuliwa kuwa miongoni mwa wajumbe wa kwanza wa baraza la seneti na Principal wa Chuo Kikuu cha Patna. Pia katika masuala yake ya sheria alikuwa akifanya kazi zake huko Bhagalpur mji maarufu kwa silk katika jimbo la Bihar.
Alizaliwa Desemba 3, 1884 huko Ziradei , India kwa wazazi Mahadev Sahai ambaye alikuwa akizungumza lugha za Kisankrit na Kiajemi na Mama yake aliyefahamika kwa jina Kamleshwari Devi ambaye alikuwa mahiri kwa kusimulia hadithi za zamani za Wahindu za Ramayana na Mahabharata. Prasad alipoanza kukua alikuwa akisimulia sana hadithio hizo na mama yake.
Katika familia yao hakuzaliwa peke yake walikuwa watano nay eye akiwa ni wa mwisho. Wa kwanza alikuwa kaka yake aliyefuatiwa na wadogo zake wa kike watatu. Licha ya kusimuliwa hadithi hakuzifaidi vizuri kwani mama yake alifariki dunia wakati akiwa bado mdogo na kaka na dada zake walianza kumtunza. Baadaye Prasad alikuja kuwa tajiri na mmiliki wa ardhi wa Kayastha. Alipokuwa mwalimu alifanya kazi katika taasisi mbalimbali.
Baada ya kumaliza shahada ya uzamili katika masuala ya uchumi alifanikiwa kuwa kupanda hadi kuwa Profesa wa lugha ya Kiingereza katika Chuo cha Langat Singh huko Muzzaffapur katika Bihar na baada akawa Mkuu wa Chuo. Prasad aliachana na chuo hicho na kwenda zake kuchukua masomo ya sheria katika chuo cha Ripon huko Calcutta ambacho chuo hicho kwa sasa kinafahamika kwa jina la Surendranath Law College.
Mnamo mwaka 1909 wakati akiwa katika masomo ya sheria huko Kolkatta alikuwa akifanya kazi kama Profesa wa Uchumi katika chuo cha Calcutta City. Mnamo mwaka 1915 alionekana katika mtihani wa shahada ya uzamili ya Sheria ambako alipita na kutunukiwa medali ya dhahabu.
Alihitimu shahada ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha Allahabad mnamo mwaka 1937. Prasad alijiunga na harakati za kutafuta uhuru wa India wakati alipohudhuria mkutano mkuu wa Chama cha Kitaifa cha India mnamo mwaka 1906.
Mkutano huo ulifanyika mjini Calcutta ambako alihudhuria kama mtu aliyejitolea kuunga juhudi za kutafuta suluhu la watu wa India. Wakati huo alikuwa akisoma pale Calcutta.Alijiunga na chama hicho mnamo mwaka 1911, katika mkutano mwingine ulifanyika hapo hapo Calcutta.
Mnamo mwaka 1916 alikutana na Mahtma Gandhi walipokuwa katika kikao cha Lucknow kilichoendeshwa na chama hicho hapo hapo Calcutta. Gandhi alimtaka Prasad aje na wenzake wanaotaka kujitolea kuunga mkono juhudi za kutafuta uhuru wa India.
Mnamo mwaka 1920 Prasad aliamua kuachana na sheria na nyadhifa nyingine katika Chuo Kikuu na kuunga mkono harakati za kudai uhuru wa India.
0 Comments:
Post a Comment