Thursday, February 27, 2020

Unaikumbuka siku iliyoweka historia kwa Maradona?

Februari 27, 1977 Argentina iliizabua Hungaria mabao 5-1 katika mchezo wa kirafiki ambao uliweka rekodi kwa mchezaji chipukizi wa Argentina Diego Maradona kuanza safari yake ya soka la Kimataifa akiwa na Albiceleste. 

Maradona alikuwa na umri wa miaka 16 katika mchezo huo. 

Aidha kwa wakati huo Hungaria ilikuwa ni timu ambayo ilikuwa na mafanikio makubwa kutokana na kufika katika fainali mbili za Kombe la Dunia mnamo mwaka 1938 na 1954. 

Pia ilikuwa timu ya taifa ambayo ilikuwa imebeba medali tatu za dhahabu za Michuano ya Olimpiki 1952, 1964 na 1968 pia walichukua medali ya fedha mnamo mwaka 1972. 

Licha ya medali hizo Hungaria ilishindwa kufuzu Kombe la Dunia mnamo mwaka 1974, michuano ya Olimpiki mnamo mwaka 1976 na Mashindano ya Ulaya mwaka 1976. 

Argentina wakati huo ilikuwa imefika fainali ya Michuano ya Olimpiki mnamo mwaka 1928 na fainali ya Kombe la Dunia mnamo mwaka 1930. Pia Argentina ilikuwa imebeba mataji ya Copa America mara 12.

Katika dimba la Bombanera jijini Buenos Aires mbele ya watazamaji akali ya 60,000 hadi mapumziko wenyeji walikuwa mbele kwa mabao manne. Mabao ya Argentina yalifungwa na Daniel Bertoni aliyefunga hat trick katika mchezo huo na mabao mawili ya Leopoldo Luque.
Akitokea benchi Zombori Sandor aliipa Hungaria bao la kufutia machozi katika dakika ya 61 ya mchezo huo.

Dakika moja baadaye kulifanyika mabadiliko Albiceleste walimtoa Ricardo Villa akaiingia Jorge Benitez na alitolewa Luque  na kuingia Diego Armando Maradona wakati huo alikuwa akihudumu na klabu ya Argentina Juniors. 
Huo ndio ulikuwa ni mchezo wake kwanza kwa Argentina na baada ya hapo alihudumu na miamba hiyo mechi 91 ana kuiongoza Argentina kutwaa Kombe la Dunia mnamo mwaka 1986.

0 Comments:

Post a Comment