Februari 28, 2010 makundi mawili hasimu katika soka nchini Ufaransa kundi la mashabiki wa klabu ya Paris Saint German walipambana tena na lile la Marseille ambapo yalisababisha kifo cha shabiki mmoja na wengine 20 kukamatwa katika vurugu hizo.
Mchezo huo ulichezwa jijini Paris ambapo PSG walikuwa wenyewe katika mchezo huo wa Ligi Kuu nchini humo maarufu Ligue 1.
PSG walikuwa wakitafuta kulipa kisasi kwani mapema mwanzoni mwa msimu huo walipoteza.
Katika mchezo huo katika dakika ya 15 winga wa Marseille Hatem Ben Arfa alikuwa wa kwanza kutikisa nyavu za PSG. Katika kipindi cha pili wageni hao walipata mabao kupitia kwa Licho Gonzalez katika dakika ya 54 na Benoit Cheyrou katika dakika ya 71 ambapo mchezo ulimalizika kwa Marseille kupata ushindi wa mabao 3-0.
Siku ilikuwa mbaya kwa mashabiki wa PSG ambao walikuwa uwanjani na waliokuwa nje ya uwanja wa Parc des Princes ambako makundi mawili ya mashabiki hasimu Boulogne Boys na Supras Auteuil yalipambana kabla ya mchezo, wakati wa mchezo na baada ya mchezo huo.
Iliwabidi polisi wa Ufaransa kutumia gesi za kutoa machozi ili kuondoa makundi hayo ambapo walifanikiwa kuwakamata mashabiki 20.
Watu wengi walipata majeraha madogo madogo, lakini mtu mmoja mwenye umri wa miaka 38 aliyfahamika kwa jina la Yann L alipata majeraha ya kichwani ambayo yalisababisha ashindwe kujitambue hadi mauti yalipomkuta majuma mawili baadaye.
PSG walinyoshewa kidole cha lawama kwa vurugu hizo ambazo ziliwafanya wasiuze tiketi katika mechi zote za ugenini katika miezi iliyobaki katika msimu huo.

0 Comments:
Post a Comment