Saturday, February 29, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Elpidio Rivera Quirino ni nani?

Februari 29, 1956 alifariki dunia mwanasheria na mwanasiasa wa Ufilipino Elpidio Rivera Quirino Mwanasia huyo aliweka rekodi ya kuwa Rais wa Sita wa taifa hilo. 

Alishika wadhifa huo kutoka mwaka 1948 hadi mwaka 1953. 

Katika siasa za Ufilipino aliingia wakati huo akiwa mwakilishi wa Ilocos Sur kutoka mwaka 1919 hadi 1925. 

Mnamo mwaka 1925 alichaguliwa kuwa seneta ambapo alidumu kwa miaka sita hadi mwaka 1931. Mnamo mwaka 1934 alikuwa mwananchama wa Kamati ya Uhuru wa Ufilipino ambayo ilimpeleka jijini Washington D.C

Baada ya kustaafu mnamo mwaka 1953 Quirino alisisitiza kuendelea kuwatumikia watu wa Ufilipino hivyo alihudumu kama "Baba wa Huduma za Kigeni." 

Qurino alifariki dunia kwa maradhi ya moyo akiwa katika nyumba yake aliyostaafu nayo ya Novaliches katika mji wenye watu wengi nchini Ufilipino.

Alizikwa katika makaburi ya Manila South katika kitongoji cha Makati katika mji mkuu wa taifa hilo wa Manila. 

Hata hivyo wakati taifa hilo liliadhimisha miaka 60 ya kumbukizi tangu kifo chake mnamo Februari 29, 2016 mabaki ya mwili wake yalihamishwa kutoka eneo lake la awali yalikohifadhiwa na kupelekwa katika Makaburi ya Mashujaa yaliyopo Taguig hapo hapo jijini Manila. 

Quirino alishinda kuongoza taifa hilo kama Rais wa sita wa Ufilipino baada kifo cha Rais Manuel Roxas mnamo mwaka 1948. 

Mara tu baada ya kifo hicho Quirino aliapishwa kushika wadhifa wa kuisimamia serikali wakati huo akiwa Makamu wa Rais mpaka uchaguz utakapofanyika. Katika uchaguzi senate Fernando López alishinda kuwa Makamu wa Rais. 

Quirino alishinda kwa kupigiwa kura na wananchi wa Ufilipino. Kwa mara ya kwanza katika ardhi hiyo Rais, makamu wa Rais na maseneta wote walitoka katika chama cha Liberal. 

Uchaguzi huo ulipingwa kila kote kwamba ulijawa na rushwa na vurugu. 

Wapinzani wa Quirino walipigwa na wengine kuuawa na waliokuwa wakimuunga mkono au polisi ambapo vitendo vya rushwa vilikuwa wazi. 

Uchaguzi wa mwaka 1953 vyama vya Nacionalitsa na Demokratiki viliunda muungano ambao ulimwangusha Quirino ambaye hali yake ya kiafya haikuwa njema. 

Msemaji wa zamani wa serikali ya Ufilipino Ramon Magsaysay aliongoza kura za wengi wa wapiga kura wapatao milioni 1.5

Wakati wa utawala wake Quirino alitangaza malengo mawili muhimu la kwanza ikiwa ujenzi imara wa uchumi wa taifa hilo  na pili kurudisha imani ya raia kwa serikali ambapo katika kuhakikisha imani ya raia wa Ufilipino wanakuwa na uzalendo kwa taifa lao; alihakikisha bima kwa wasiokuwa na ajira, bima ya uzeeni, bima ya ajali na ulemavu wa kudumu, bima ya afya, bima ya uzazi, nafasi za kazi.

0 Comments:

Post a Comment