Mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika mikoa minne ya Lindi, Mwanza, Morogoro na Manyara nchini Tanzania, imesababisha vifo vya watu 40.
Maofisa wanasema mafuriko yamesomba nyumba takriban 1,750 na kusababisha watu zaidi ya elfu 15 kupoteza makazi. Wameongeza kuwa watu 21 wamefariki mkoani Lindi, watu saba wamekufa wilayani Mvomero na Malinyi mkoani Morogoro wakiwemo watoto watatu, watu watatu wamefariki wilayani Bahati mkoani Manyara, na watu tisa wamekufa mkoani Mwanza.
Meneja mkuu wa shirika la reli ya Tanzania Masanja Kadogosa amesema shirika hilo limesimamisha huduma kati ya Morogoro na Dodoma kutokana na mafuriko.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa ya Tanzania inasema mvua kubwa itaendelea kunyesha kwenye maeneo mengi nchini humo katika saa 24 zijazo.
0 Comments:
Post a Comment