Wednesday, February 12, 2020

Unaikumbuka siku Ricardo Kaka alipopewa uraia wa Italia?

Februari 12, 2007 nyota wa zamani wa klabu ya AC Milan na timu ya taifa ya Brazil Ricardo Kaka alibadili uraia wake na kuwa Muitaliano. Licha ya kubadili uraia wake aliendelea kulitumikia taifa la Brazil. 

Alijiunga na AC Milan 'Rossoneri' mnamo mwaka 2003 kwa misimu miwili akitokea Sao Paulo ya Brazil. Rossoneri walilipa Euro milioni 8.5 na kwa haraka zaidi alifanikiwa kufumania nyavu mara 14 katika mechi 44 alizocheza  katika mwaka wake wa kwanza aliotua. 

Kaka alifanikiwa kutwaa taji la Supercoppa Italia na mnamo mwaka 2004 alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa Mwaka wa Serie A. 

Alianza kwa nguvu msimu wa 2006-07 ambao ulimfanya mwishoni mwa mwaka 2007 atwae tuzo ya Ballon d'Or. 

Katikati ya msimu huo aliamua kuomba uraia wa Italia ambapo aliupata rasmi Februari 12 na baada ya kupokea alifanya sherehe yake binafsi kwa kupata uraia huo. 

Kupata uraia huo haukuwa na madhumuni ya kuharibu hadhi yake ya kimataifa kwani alikuwa tayari ameshazuiliwa kucheza katika timu za Brazil na Italia.

Isipokuwa kupata uraia huo kulikuwa na manufaa makubwa kwa klabu ya AC Milan ambao walipeleka kilio chao cha kuwa Kaka ni mchezaji aliyepo katika Umoja wa Ulaya.

Alisalia na klabu ya AC Milan hadi Juni 2009 ambapo alijiunga na Real Madrid. Mnamo mwaka 2014 alikwenda zake Marekani ambako alihudumu na Orlando City hadi kustaafu kwake mnamo mwaka 2017. 

Timu ya taifa ya Brazil aliitumikia kwa miaka 14 kutoka mwaka 2002 hadi 2016 akicheza michezo 92 na kufunga mabao 29.

0 Comments:

Post a Comment