|
Nyota wa Tanzania na klabu ya Aston Villa Mbwana Samatta akifunga bao lake la kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England dhidi ya AFC Bournemouth licha ya Aston Villa kupoteza kwa mabao 2-1. Samatta alitua Villa Park akitokea Genk ya Ubelgiji. Huo ni mchezo wa pili wa Samatta tangu alipokanyaga ardhi ya England. Mchezo wake wa kwanza ulikuwa wa Kombe la Ligi dhidi ya Leicester City uliowapeleka fainali ya EFL 2019/2020 ambapo watakutana na Manchester City Machi 1, 2020. |
0 Comments:
Post a Comment