Februari 10, 2012 alifariki dunia mwanamuziki, mcheza filamu na mwanamitindo wa nchini Marekani Whitney Houston.
Mwili wake ulikutwa katika chumba cha hoteli ya Beverly Hilton huko Beverly Hills, California.
Mama yake Whitney, Cissy Houston alikuwa mwimbaji wa nyimbo za injili, na ni binamu yake mwimbaji Dionne Warwick.
Mkongwe wa soul Aretha Franklin (Machi 25, 1942 – Agosti 16, 2018) ni mama wa ubatizo wa Houston.
Msingi wa muziki wa Houston ni miondoko ya soul na nyimbo za injili.
Alianza kuimba kanisani na aliwahi kuwa mwanamitindo kabla ya kuingia mkataba na kampuni ya kurekodi muziki ya Arista.
Miaka ya mwishoni mwa maisha mwake, matumizi ya dawa za kulevya yalimzidi msanii huyu na sauti yake nyororo kuharibika.
Houston alikuwa na nyimbo zilizovuma katika miaka ya 80 na mapema miaka ya 90. Lakini fani yake ilighubikwa na matumizi ya dawa za kulevya na ndoa yake yenye mtikisiko kwa mwimbaji Bobby Brown.
Katika kilele cha fani yake miaka ya 80 na 90 alishinda tuzo nyingi na kutoa nyimbo zilizovuma kama vile I Will Always Love You na Didn't We Almost Have it All.
Msanii huyu alikuwa mmoja wa wasanii maarufu wa kike duniani. Pia aliweza kucheza filamu kadhaa kama vile The Bodyguard na Waiting to Exhale.
Alizaliwa Agosti 9, 1963 Newark, jijini New York na kufariki dunia Februari 11, 2012. Nyota huyo aliwahi kutwaa tuzo ya Grammy akiwa mwimbaji bora wa Pop/R&B, mwigizaji. Mtayarishaji wa filamu, mtunzi wa nyimbo.
Alifahamika zaidi kwa kuwa sauti kali yenye nguvu na mvuto. Miongoni mwa nyimbo zake ni "I Will Always Love You" na "I wanna dance with some body" kutoka katika toleo lake la 'The Star Spangled Banner.'
Whitney ni mmoja kati ya wasanii wa kike waliopata mafanikio makubwa kabisa katika medani ya muziki.
0 Comments:
Post a Comment