Tuesday, February 25, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Jersey Joe Walcott ni nani?

Februari 25, 1994 alifariki dunia mwanamasumbwi  wa Marekani Jersey Joe Walcott. 

Siku  aliyopoteza maisha ilikuwa Ijumaa, maradhi ya kisukari yalimuondoa nyota mwanamasumbwi huyo akiwa katika hospitali ya Our Lady of Lourdes Medical Center mjini Camden huko New Jersey.

Jersey Joe mtoto wa wahamiaji maskini kutoka Barbados ambaye alikulia katika umaskini huo na baadaye kuweka rekodi vitabuni kwa mchezaji mwenye umri mkubwa kushinda taji la uzito mkubwa la dunia alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.

Binamu yake aliyefahamika kwa jina la Richard Cream ndiye aliyethibitisha kifo cha mwanamasumbwi. 

Jina lake halisi lilikuwa Arnold Raymond Cream. Alikuwa akifahamika kutokana uimara wake kwa asili na mwanamichezo ambaye alikuwa akimaanisha katika fani yake.

Jersey Joe hakuondoka katika medani hiyo ya uzito wa juu mpaka alipotwaa taji hilo baada ya kushindw akulitwaa kwa mara nne.

Aliwahi kukaririwa mara kadhaa akisema, "I always felt in my heart that God would give it to me."

Julai 18, 1951 akiwa na umri wa miaka 37 alimtandika Ezzard Charles ambaye alikuwa amemzabua mara mbili.

Katika raundi ya saba ya pambano hilo pale Forbes Field mjini Pittsburgh alifanikiwa kuweka rekodi hiyo ambayo inaelezwa ilikuja kuvunjwa na George Foreman mnamo mwaka 1994 kwa kutwaa taji la uzito huo akiwa na umri wa miaka 45. 

Jersey Joe alifahamika sana kutokana na kumtandika mara tatu mwanamasumbwi mahiri Joe Louis. Alimtandika Desemba 5, 1947 pale Madison Square alimpomzambua kwa KO mara mbili.

Mwanamasumbwi huyo alishindana kati ya mwaka 1930 hadi 1950. Alishikilia taji la uzito wa juu katika ya mwaka 1951 hadi 1952.

Alicheza mapambano 71 akishinda 51 na kupoteza 18. Mapambano mawili ya mwisho alitandikwa vibaya sana kwa KO na Rocky Marciano Mei 15, 1953 mjini Chicago, Illinois baada ya lile lililochezwa Septemba 23, 1952 Philadelphia, Pennsylvania.

Baada ya kustaafu masumbwi Jersye Joe hakuweza kwenda mbali sana na medani hiyo akaingia katika kucheza filamu na vipindi kadhaa vya televisheni.

Alikuwa mwamuzi wa mapIgano mbalimbali baada ya kustaafu kwake lakini baada ya mkanganyiko katika pambano lililowakutanisha Muhammad Ali na Sonny Liston Februari 25, 1964 ambapo Muhammad Ali alizabuliwa katika raundi ya saba wakati huo alikuwa hajabadili jina lake la Cassius Clay. 

Pambano hilo lilipigwa pale Miami Beach, jimboni Florida baada ya hapo hakuitwa tena kuamua mapambano hayo. 

Kutoka mwaka 1971 hadi 1974 Jersey Joe  alichaguliwa kuwa polisi katika Kaunti ya Camden, New Jersey na aliweka rekodi ya kuwa Mmarekani wa kwanza mweusi kushika nafasi hiyo katika kaunti ya Camden. 

Kutoka mwaka 1975 hadi 1984 Jersey Joe alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Jimbo la New Jersey.

0 Comments:

Post a Comment