Wednesday, February 5, 2020

MAKTABA YA JAIZMELA: Shunzhi ni nani?



Februari 5, 1661 alifariki dunia Mtawala wa China aliyefahamika kwa jina la Shunzhi (Shizu). Shunzhi alikuwa mtawala wa tatu kutoka katika ukoo wa Qing. 

Pia ndiye mtawala wa kwanza kuitawala China yote vizuri. Aliitawala China kutoka mwaka 1644 hadi 1661. Kamati ya Maprinces wa Manchu ilimteua kukalia nafasi hiyo baada ya kifo cha baba yake Hong Taiji aliyefariki dunia wakati Shunzhi akiwa na umri wa miaka mitano  Septemba 1643. Hong Taiji alizaliwa mwaka 1592. Wakati huo huo waliwateua wengine wawili kutoka katika ukoo wa Kifalme ili kumsaidia Shunzhi hadi atakakuwa na uwezo wa kusimama na kuongoza. Dorgon (1612-1650) ambaye alikuwa ni mtoto wa 14 wa mwanzilishi wa ukoo wa Qing Mzee Nurhaci (1550-1626). Na mwingine alikuwa Jirgalang (1599-1655). Kutoka mwaka 1643 hadi 1650 mamlaka yote ya kisiasa yalikuwa mikononi mwa Dorgon. Wakati wa utawala wake alifanikiwa kuipanua Dola ya Qing kwa kuteka ukoo wa Ming na kuuangusha kabisa ambao ulidumu kwa takribani karne tatu kutoka mwaka 1368 hadi 1644. Pia Dorgon alifanikiwa kuwatimua na kuwasukumia katika majimbo ya China huku akiwalazimisha kunyoa nywele  na kusalia na upara. Sheria hiyo ilidumu hadi kifo chake Dorgon mnamo mwaka 1650. Shunzhi alipokea mikoba hiyo lakini alijitahidi kuendelea mafanikio ya Dorgon, alipambana na rushwa na alipunguza ushawishi wa Machu katika kuamua masuala ya taifa hilo. Akiwa katika utawala huo mnamo mwaka 1661 majeshi yake yalipata upinzani kutoka katika ukoo wa Ming na kumshinda. Adui wake wa mwisho walikuwa Koxinga (1624-1662) na Prince Gui (1623-1662) kutoka majimbo ya Kusini ambako ukoo wa Ming ulisukumiziwa huko. Shunzhi alifariki dunia kwa ugonjwa wa ndui akiwa na umri wa miaka 22. Ugonjwa huo uliitesa sana China hususan wale ambao hawakuwa na chanjo wakati huo wakiwamo Machus.

0 Comments:

Post a Comment