Friday, February 21, 2020

Hatasahaulika chipukizi Duncan Edwards la Manchester United

Februari 21, 1958 nyota wa klabu ya Manchester United aliyekuwa na umri wa miaka 21 alifariki dunia kwa ajali ya ndege iliyotokea Minich nchini Ujerumani. 

Duncan Edwards  alikuwa miongoni mwa nyota chipukizi waliingizwa katika kikosi cha wakubwa. Alifariki dunia kutoka na majeraha makubwa yalihitimisha pumzi yake. 

Alijiunga na Mashetani Wekundu mnamo Juni 1952 katika programu ya vijna na mwaka mmoja baadaye alisaini mkataba wa kuhudumu na timu ya wakubwa. 

Kocha wa Manchester United wakati huo alikuwa Matt Busby ambaye alimpa nafasi katika kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Cardiff City katika mchezo uliochezwa katika dimba la Old Trafford. 

Wakati akipewa nafasi hiyo ya kuwamo Duncan Edwars alikuwa na umri wa miaka 16 na siku 185 hivyo kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mdogo kucheza katika ligi hiyo. 

Katika mchezo Manchester United ilipoteza mchezo huo baada ya kukubali kibano cha mabao 4-1. 

Wengi walimuona Duncan Edwards na kuongeza kuwa kipaji chake kitakuwa na maana zaidi siku za usoni. Mchezaji mwenzake Bobby Charlton ambaye ni mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or mnamo mwaka 1966 alimzungumzia Duncan kuwa ndiye mchezaji pekee aliyekuwa akimfanya anyong'onyee. 

Kabla mauti hayajamkuta alikuwa ameshacheza mechi 24 katika msimu wa 1953-54. Mnamo Aprili 1955 aliweka rekodi nyingine ya kuwa mchezaji  wa kwanza kucheza timu ya taifa akiwa na umri mdogo ambapo Duncan Edwards alicheza  akiwa na umri wa miaka 18 na siku 183. 

Baada ya hapo nyota huyo alicheza mechi 18 kwa miaka mitatu. Hata hivyo Februari 6, 1958 jijini Munich maisha ya nyota huyo yalikatishwa baada ya ajali hiyo. 

Wachezaji saba walipoteza maisha papo hapo huku Duncan na kocha Busby wakiwawahishwa hospitalini kwa ajili ya matibabu. Manchester United ilitoka kucheza mchezo dhidi Red Star Belgrade katika Kombe la Ulaya. 

Duncan Edwards alifariki dunia majuma mawili baadaye ambayo ilikuwa Februari 21 na kocha Busby alipata nafuu na kuruhusiwa.


0 Comments:

Post a Comment