Februari 24, 1992 nyota wa soka wa England na mkongwe wa klabu ya West Ham Robert Frederick Chelsea Moore OBE maarufu Bobby Moore alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 51 kutokana na maradhi ya saratani ya kibofu cha mkojo.
Moore alianza soka lake mnamo mwaka 1958 akiwa na West Ham ambapo alisalia kwa zaidi ya miaka 15 Mashariki mwa London.
Licha ya kwamba Moore alikuwa na kipaji cha wastani lakini alikuwa na uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo na kujua namna mwelekeo wa mpira unakwenda pasipo kuwa na mpira kwa wakati mwafaka.
Hali iliyomfanya aonekana mchezaji mkubwa wa England na mlinzi mwenye kiwango cha juu wa taifa hilo. Akiwa na umri wa miaka 21 aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa. Akiwa na umri wa miaka 22 alipewa unahodha wa kikosi cha England.
Taji lake la kwanza ilikuwa mwaka 1964 akiwa na West Ham walipotwaa Kombe la FA pia mwaka huo huo alichukua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kutoka Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini England.
Pia Moore aliisaidia West Ham kutwaa Kombe la Washindi mnamo mwaka 1965 kwa kuizabua 1860 Munich kwa ushindi wa mabao 2-0.
Anakumbukwa sana na wapenzi wa soka wa England pale alipoiongoza timu yake ya taifa kutwaa Kombe la Dunia mnamo mwaka 1966 ambapo Moore alitengeneza mabao mawili katika ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Ujerumani katika fainali.
Alihudumu na England takribani mechi 108 na kuwa miongoni mwa wachezaji wa England waliocheza mechi nyingi wakiwa na miamba hiyo wengine ni Peter Shilton (125), Wayne Rooney (120), David Beckham (115), Steven Gerrard (114) na Bobby Moore akishika nafasi ya tano katika orodha hiyo kwa sasa.
Aliondoka West Ham mnamo mwaka 1974 na kwenda Fulham waliokuwa daraja la pili wakati huo. Akiwa na Fulham katika msimu wake wa kwanza pale Craven Cottage walikutana na West Hama mara mbili katika Kombe la Ligi.
Katika maisha yake ya soka aliwahi kwenda kuhudumu na San Antonio Thunder na Seattle Sounders nchini Marekani kabla ya kustaafu mnamo mwaka 1978.
Katika maisha yake ya soka Bobby Moore alicheza mechi 716 na kufunga mabao 26.
Katika masuala ya uongozi alikaa muda mchache sana akipendelea zaidi kuwa mtangazaji wa mechi za soka.
Wiki moja kabla ya kufariki kwake alitangaza kwa mara ya mwisho katika mchezo baina ya England na San Marino Februari 17, 1993
0 Comments:
Post a Comment